Nuh Mziwanda amewataka wasanii kuwa
wazalendo kwa kuonyesha hisia zao za vyama vya siasa na kuonyesha
ushirikiano katika kuhamasisha. Akizungumza na Planet Bongo ya East
Africa Radio, Nuh alisema maendeleo yatakayopatikana ni manufaa kwa
watanzania wote kwa ujumla.
“Wewe ukiwa msanii sio kwamba sio mwananchi wa kawaida,” alisema.
“Wewe pia unahitaji kutawaliwa
vizuri. Unahitaji utawala mzuri ambao utaongoza hata kazi zako ziende
vizuri. Kwahiyo ni vyema mtu ukajua upo... upande gani. Huo ni upendo wa
nchi yako na ni mzalendo. Kila binadamu anapenda uongozi mzuri ndio
maana kila mtu akiwa na akili timamu ana haki ya kuchagua chama
anachokitaka,” aliongeza.
“Lakini sisi wasanii tusijisahau
tukawa tunashindwa kuweka hisia zetu kwaajili ya maslaHi ya nchi yetu.
Unaogopa kuweka wazi wewe ni chama gani, unampenda mwanasiasa gani! Sisi
ni vioo vya jamii tunaangaliwa pia na watu na kuna watu wahitaji
ushauri au ufafanuzi juu ya viongozi waliotangaza nia. Kwa sisi
inatubidi tuwe mfano kwanza kabla ya wananchi.”
Wednesday, September 9, 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment