Friday, November 20, 2015
LIST YA WASANII WA BONGO WALIO ANZIA MUZIKI KANISANI
Tukiangalia game la muziki nchini kwetu tuna historia pia za namna hii, wasanii mbalimbali wameelezea kitu kama hiki na sio kitu kigeni sana kukisikia, katika muziki wa kizazi kipya na wapo ambao tumewaona wakielezea imekuwaje vigumu kwao kutoka kanisani na kufanya mziki wa kidunia na hawa ni wasanii ambao walianza mziki kanisani. 1: Linah Sanga, 2: Vanessa Mdee, 3...
Baraka Da Prince
Baraka ametokea katika familia ya wasabato, na upande wa mama yake pamoja na wajomba zake ni watu wanaoimba sana na kupiga vyombo mbalimbali vya muziki kanisani, yeye pia safari hii ya muziki aliianza kanisani kwa kuimba kwaya.
Vanessa Mdee
Vanessa kwa hali ya kawaida tu ukimuangalia huwezi amini kama ni mtoto wa mama mchungaji, safari ya mziki wa Vanessa ilionekana ya ghafla kwa wengi hasa baada ya kutoa ngoma nzuri mfululizo toka alipoanza mziki hadi sasa,lakini ukweli ni kwamba Vanessa pia alianzia kanisani kwa kuimba kwaya.
Ruby
Ruby niliona mahojiano yake na Sporah kwenye The Sporah Show na historia yake yeye kidogo ni tofauti sababu sio tu kuimba kanisani bali yeye aliishi huko huko kanisani pamoja na watumishi kibao wa nyumba ya ibada,Lakini bado mziki wa kidunia mlimteka na kuamua kuhamisha majeshi yake kidunia zaidi.
Jokate Mwengelo
Kwa upande wa mrembo huyu mwenye vipaji lukuki kama kuigiza,urembo,biashara, lakini pia anaimba, Jokate alikuwa anaitwa Mlokole japokuwa ni jina lililokuwa likitumika kama kumkashifu baada ya yeye kuwa katika mahusiano na Diamond, lakini hayo si muhimu sasa, ila kama msanii na muimbaji safari yake pia ina historia ya kuanzia kanisani.
Linah Sanga
Familia ya Linah ni familia iliyojengeka kikristo, kwa malezi na maadili yote ya kidini na safari ya Linah pia kimuziki ilianzia katika kundi la kwaya kanisani,na yeye pia alisha thibitisha hilo.
Judith Wambura
Lady Jay Dee, komando kwa upande wake ilisemekana alitengwa hadi na kanisa kwa kosa la kuacha kufanya kazi ya mungu na kuimba nyimbo za kidunia,baada ya kuacha kuimba kwaya na kuingia katika bongo fleva,komando kama lilivyo jina lake bado alisimama kama mwanamke aliefanikiwa katika mziki kuliko wanawake wengine walioanza nae mziki miaka ya nyuma.
Labels:
HABARI & UDAKU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment