Pages

Subscribe:

Tuesday, November 17, 2015

KAULI YA H-BABA BAADA YA KUONA HAPATI TUZO

Msanii wa Filamu na Muziki aina ya Afro Pop hapa Tz maarufu kwa jina la H Baba ambaye ni mume wa Flora Mvungi, mwenye utaratibu wa kuandaa tuzo katika familia yake Amepiga story na mwandishi wetu kuhusiana na yeye kuendelea kuzikosa tuzo za Muziki hapa nchini mara baada ya kupigwa maswali machache hapa anafunguka zaidi.

“Unajua inatia hasira sana, sasahivi wasanii wenye vipaji ndio wanawekwa pembeni wanachukuliwa wasanii wasio na vipaji, unamnyimaje tuzo ya heshima mtu kama...
Mr.blue ambaye yeye kawabadilisha wasanii wote kuvaa wasanii tulikuwa hatujui kuvaa kabisa unakuta tunavaa mashati makubwa maviatu makubwa, lakini Mr. Blue katubadilisha hatatuzo!.

Mnafahamu kuwa kwenye stage hakuna msanii anayeniweza niliwahi kutangaza na ninatangaza tena msanii yeyote Yule ambaye anajiona ananiweza kwenye stage ajitokeze, mimi nitaperform bure, yeye alipwe pesa, hakuna aliye jitokeza na sidhani kama atajitokeza nakama yupo hata sasahivi nipo tayari kwa hilo.

Kwa style hii tunaua muziki wa Bongo coz tunatanguliza bahasha za pesa mbele kuliko kazi, tunatengeneza Team kwenye mitandao kwa kutumia pesa kwa ajili ya kutukana wasanii wengine huo si upuuzi!, tunapoteza vipaji vya madirector wa Bongo, tunaenda kuwanufaisha na kuwapa Kiki Madirector kwenye nchi za watu inauma sana”

0 comments:

Post a Comment