Member wa kundi la Navy Kenzo na mtayarishaji wa muziki, Nahreel
amesimulia maisha na mpenzi wake Aika wanayeunda naye kundi hilo. Kabla ya kuanzisha kundi la Navy Kenzo, wawili hao walikuwa wakiunda kundi la Pah One na wasanii wengine wawili.
“Mimi na Aika tumekutana tukiwa India masomoni, wote tulikuwa
tunasomeshwa na wazazi wetu, tumepitia mambo mengi sana tukamaliza shule
na tukaja Tanzania,” Nahreel alikiambia kipindi cha Mkasi cha EATV.
“Mimi nikawa nimeajiriwa na Aika akawa
ameajiriwa lakini baadaye tukaona muziki wetu unapotea, kwa sababu
tumeingia kwenye kazi nyingine. Kwahiyo tukaamua kuja Dar ili... kufanya
mambo ya muziki,” aliongeza.
“Kwahiyo tulianza chini sana, tulianza with
nothing, nilikuwa na godoro dogo ambalo nilianza na Aika. Tulikuwa
tunalala kwenye hilo godoro mimi na Aika. Tukaanza hivyo huku tunafanya
muziki. Mimi nafanya production zangu na Aika anafanya shughuli zake za
mitindo ndio hivyo tumetokea kwenye vitu vingi tukajenga mpaka hapa
tulipofika.”
“Tumepambana sana mpaka kufikia hapa.”
Wednesday, November 11, 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment