Mwanamke aitwaye, Asma Jama ameshambuliwa nchini Marekani kwa kuongea Kiswahili. Jama alikuwa amekaa na familia yake kwenye mgahawa wa Applebee huko
Minnesota, akikata kiu na juice huku mazungumzo yakiendelea kabla ya
kujeruhiwa vibaya mdomoni. Mwanamke aliyekuwa amekaa jirani yake
alimponda... na glasi nzito ya bia mdomoni.
Sababu? Jama alikuwa akizungumza Kiswahili na familia yake.
“Siamini baada ya miaka yote hii mtu ananipiga
sababu niko tofauti,” alisema Jama. “Mtu ananipiga kwasababu nilikuwa
nikizungumza lugha ya kigeni.”
Shambulio lilimwacha Jama na majeraha usoni pamoja na mdomo kuchanika kiasi cha kushonwa nyuzi 17.
Jodie Burchard-Risch, 43, na mume wake, walikuwa wamekaa kwenye mgahawa
huo jirani na Jama, aliyekuwa ameketi na binamu na watoto wa nduguze.
Wawili hao walichukizwa baada ya kumsikiliza Jama na familia yake
wakizungumza lugha ngeni.
Jama alisema wawili hao waliwaambia waende nyumbani. “Walisema ukiwa Marekani unatakiwa kuzungumza Kiingereza.”
Jama, ambaye ni msomali, alihamia Minnesota mwaka 2000 kutoka Kenya. Anazungumza lugha: Kiingereza, Kiswahili na Kisomali.
Jumatatu hii, Burchard-Risch alishikiliwa kwa kosa la shambulio.
Kutokana na shambulio hilo, Jama anadai hana amani tena na anafikiria
kuhama Minnesota. Amesema anaweza kuungana na dada yake aliyehama
Minnesota mwezi June na kwenda Dallas.
Monday, November 9, 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment