Shilole amekanusha kujihusisha na kusafirisha madawa ya kulevya katika
safari zake za nje lakini amekiri kuwahi kushawishiwa kufanya hivyo. Muimbaji huyo alikiambia kipindi cha Planet Bongo cha EATV kuwa alikataa mtego huo kwakuwa hakupenda kuhatarisha maisha yake.
“Kiukweli ushawishi upo niache kusema uongo
lakini kwa sababu binafsi na akili zangu timamu na najua nini nafanya
basi huwa naweka tamaa pembeni na kuangalia... kitu ambacho kina mwendelezo
na maisha yangu,” alisema.
“Nikiwaangalia watu halafu nikiangalia mpenzi
wangu ninavyompenda nimwache hivi hivi, roho inauma pamoja na watoto
wangu, nawapenda sana. Halafu wananipa matumaini kwa sababu wana akili
sana shuleni,” alisisitiza.
Wednesday, November 11, 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment