Pages

Subscribe:

Friday, November 6, 2015

LINEX: NIMESHA CHAPWA SANA NA MAMAYANGU KWA SABABU YA AIFOLA



Kama ulikuwa hujui kuhusu wimbo wa Aifola wa msanii Linex, fahamu kuanzia sasa kuwa jina la Aifola sio la mtu bali ni eneo ambalo msanii Linex alikuwa anapenda kwenda kuogelea alipokuwa mdogo. Linex ameyasema hayo jana alipokuwa akiongea na Planet Bongo ya East Africa Radio na kueleza kuwa mama yake alishawahi kumchapa sana kwa kupenda kwenda eneo hilo la Aifola.

"Aifola ni eneo ambalo mi nilikuwa naogelea wakati niko mdogo, yani ni beach inaitwa Aifola, kwa hiyo Aifola ilikuwa ni nyimbo flan tulikuwa tukiimba wakati tuko...
beach kushindana kuogelea, tulikuwa tukiimba Aifoola Aifoola, kwa hiyo Aifola haikuwa jina la mtu ilikuwa ni jina la eneo ambalo mi nilikuwa naogelea na nimeshachapwa sana na mama yangu kwa ajili ya kwenda hiyo sehemu", alisema Linex.
Pamoja na hayo Linex amesema hata wazo la kufanya kazi na Fundi Samweli kwenye wimbo huo aliipata kwa kuwa alipenda kazi yake aliyofanya na Lord Eyes, hivyo akavutika kufanya naye kazi.
"Kitu kingine why nilifanya na Fundi ile ilitokea tu automatic, kwa sababu nakumbuka nilianza kumsikia Fundi kwenye wimbo aliofanya na kina Lord Eyes na G Nako, nikapendezwa na production yake nikatafuta namba yake tukawa tunawasiliana, Fundi pia kumbe alikuwa anapenda muziki wangu, anapenda ninavyoimba, kwa hiyo tukaarange siku moja, tukatuna studio tukatengeneza beat, tukarekodi siku hiyo hiyo", alisema Linex.

0 comments:

Post a Comment