Muimbaji
wa muziki wa R&B aliyewahi kupata dhoruba la kufungiwa kwa video ya wimbo
wake ‘Uzuri Wako’ na Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) kwa kigezo cha maadili,
ameeleza jinsi kigezo hicho kinavyoathiri wasanii na kushindwa kupiga hatua.
Jux
aliyeachia video ya wimbo wake mpya ‘One more Night’ hivi karibuni, amekiambia
kipindi cha FNL kinachoruka kupitia EATV kuwa, kama wakiendelea kubanwa na
kigezo hicho, wasanii wa Tanzania watashindwa kushindana na...
wasanii wa
kimataifa.
“Unajua
muziki wetu bado ni mchanga sana kwa hiyo tukisema kila kitu kiwepo kama
tunavyotaka sisi Watanzania ni ngumu sana. Kwahiyo sometimes sisi kama wasanii
tunaofanya muziki tukitaka tuendelee mbele, kama mtu unasema unataka kuwa
international halafu unafanya kazi za kitanzania huwezi kwenda mbele,” alisema.
“Kwahiyo
kama unataka kazi yako iwe international unatakiwa uamue kufanya kitu ambacho
shabiki kitamvutia na kina uhalisia. Tunatoa pesa nyingi sana kwenye video,
tunataka video zetu ziende mbali zaidi na watu ambao wanataka kuona wanataka
kuona ni kitu gani ambacho unaimba na jinsi gani kinaendana na matendo ya
video, kwahiyo ukisema tuweke utanzania, haina maadili haina nini hatuwezi
kwenda popote. Kuna vitu ambavyo hatutakiwi kivipitiliza vya kawaida.”
Video
zingine zilizowahi kufungiwa kupigwa kwenye TV kwa kigezo cha maadili ni ‘Sugua
Gaga’ ya Shaa, ‘Kabinti Special’ ya Dully Sykes na zingine.
0 comments:
Post a Comment