Inawezekana ni muda mrefu sana haujamsikia Ommy Dimpoz akizimiliki
headlines kwenye ma Radio na TV, sasa time anatarajia kuachia single
mpya iitwayo Achia Body iliyotayarishwa na Man Water & Mo Fire.
Akiongea na ripota wa millardayo.com alisema:’Baada ya kimya cha muda
mrefu kutokana na tours zangu kwahiyo imepita kipindi kirefu sana
mashabiki zangu walikuwa wanasubiri ujio wangu ndio maana nikaona sio
vibaya kuwapa zawadi ya... kufungia mwaka pamoja na sikukuu ya
Chrismas’>>> Ommy Dimpoz
‘Ndio maana nimeamua kuachia rasmi hii single yangu iitwayo Achia Body
imetayarishwa na Man Water & Mo Fire, video nimeshoot Afrika Kusini
kikubwa tu zaidi watu wajiandae kucheza muziki mzuri kwahiyo ni ngoma
ambayo itawapa watu furaha, na kesho ndio siku ambayo nitaizindua video
ya single hiyo mpya pale AKEMI Golden Jubilee Town Dar es
Salaam‘>>>Ommy Dimpoz
0 comments:
Post a Comment