Roma
anahisi mfumo wa vyombo vya habari kulipa mirahaba kutokana na uchezaji kazi za
wasanii utakaoanza January utachimba kaburi kwa muziki wa Tanzania.
Tunaingia katika vita ambayo tutawapoteza wapiganaji
wetu wengi sana mahiri na wale watakaosalimika ni wachache sana!! Na sio kama
watasalimika kwakuwa wanajua saaaana kupigana au wanazijua mbinu za kivita No.
Ni kwakuwa tu walipewa...
silaha zote za kujilinda na kupambana!!
Na hawa mahiri waliingia vitani wao kama wao na Mungu
wao bila kupewa silaha yoyote ile!!
RADIO/TV PROMOTION
Radios/Television watakuwa wanatumia vigezo gani
kuchagua kuwa hii bidhaa tuinunue na hii tusiinunue? Ilhali hadi sasa hizo
bidhaa zipo tu mtaani zimezagaa tena nyiiingiii saaana za kila ainaaa na za
kila ladha na zinapatikana Bureeee!!! Na Wakati Mwingine Radio/Tv Station
Inachukua Bidhaa hizo kwa Interest Zao Pasi hata Wadau kujua kuwa
iliyochukuliwa ni nzuri sana kuliko zingine au iliyoachwa ndiyo ingeuza zaidi
sokoni!! Na hadi inafkiaga wakati RADIO/TV zinakataa kuzichukua bidhaa hizo!!
Na inaweza ikachukua lakini ikazitumia kwa siku chache tu na kukimbilia bidhaa
nyingine!!
Hivi, tuwaze tu kimaskini hapa Ni nani akisikia swala
au neno KULIPWA/MALIPO/MTALIPWA Ni nani Atachomoa!!? Nani anakataa pesa!!?
Lakini unahisi kwanini katika hili wapo watu wengi tu WANASITA!? Nani anasita
mbele ya pesa!!? Ni kwasababu KUNAYO NAMNA tu Hapa!! Kwani tungeambiwa Jamani
kuanzia January Mkifanya SHOW Popote Pale Mnalipwa Kwanza na Taasisi flani!!
Kisha ndio promota anakulipa pia!! Nani angebisha? Sana sana Swali la kwanza
lingekuwa WANATOA NGAPI!!? hakuna asietaka hela!! Ila inakuja kwa njia gani!!??
Miongoni mwa vilio vikubwa vya wasanii wengi hasa
WACHANGA na hasa hasa WAKONGWE ni PROMOTION!!!
Wasanii tunalilia promotions wakati mwingine
TUNALIPIA kabisa ili tutangaze bidhaa zetu(nyimbo)na hili tu lilikuwa gumu sana
hadi kupelekea wasanii kupotea kwenye ramani/ wengine kuwa na uhasama na vituo
vya tv/radio au watangazaji/djs…. wengine kuwa frustrated na hili hadi kumess
up na mashabiki!! Na mifano mingine mingi mibaya!! Haya yote yalitokea pindi
msanii anapoikosa Promotion!!
Wapo wasanii walipotea kwa kipindi na wakaweza kurudi
vizuri hadi sasa hivi ni vinara na wanafanya vema!!na Wameajiri vijana wengi
kupitia kurudi kwao!! unadhani kwanini!!?? Ni PROMOTION tu imewarudisha ambayo
ni nzuri sana! Je wapo wangapi ambao wana ndoto za kurudi!!? Na Inawezekana!!
Je mnataka Ndoto zao zisitimie tena!!?
Unadhani Radio/Tv station kwa sasa zinaweza zitaamua
kupromote kumrudisha msanii tena kwa kumlipa wao kama radio!? Yaani mtu yupo
nyumbani kwake hasikiki tena….alishatoa ngoma tatu mfululizo zimekataa kisha
tumfate tumwambie sasa tunakulipa toka kwako twende ukafanye
kazi!!?Tunakupromote na tunakulipa!!Si atasema ZALI LA MTENDE Hili!!
Itawezekana kweli?
AU NDIO INAKUWA ILE YA ALIEPOTEA NDIO KASHAPOTEA
HARUDI TENA!!? Ambayo haitakiwi kuna watu wana vipaji kwa Sanaa yetu ilivo
wanahitaji sana nafasi za pili pasipo Mipaka kama hii tunayotaka kuwawekea!!
Sasa leo ikiwekwa kuwa Television/Radio Ikipiga kazi
ya Msanii Imlipe!! Msanii yule yule ambae mimi tu kama Radio Ananililiaga
nimpigie Bure na Sipigi!!Leo NIMLIPE!!? Sawa pesa za kulipwa wasanii
zipo/Sheria inaruhusu pia!! Tatizo Radio/Tv station WAPO TAYARI!!? Kwa sasa!!?
Na Je Radio zote hadi Hasa hizi Local za mikoani!!?
Ambazo zipo nyingi sana na Kila siku zinalalamika
Hazipati MATANGAZO!
Local Radio nyingi zinashindwa kuwalipa Mishahara wafanyakazi wao/ watangazaji/Madjs kwasababu wanalalamika Radio Haiwaingizii Pesa kupitia matangazo!! Je Wataweza kuendesha radio na kulipa Wasanii!!???
Local Radio nyingi zinashindwa kuwalipa Mishahara wafanyakazi wao/ watangazaji/Madjs kwasababu wanalalamika Radio Haiwaingizii Pesa kupitia matangazo!! Je Wataweza kuendesha radio na kulipa Wasanii!!???
TUZO
Kutakuwa na sheria za kuzitaka radio zinunue kazi za
wasanii wote bila interest zao kama radio. Maana Kama radio inaamua Inunue
Ngoma za Stamina Na Kala tu na kuzipromote hizo hizo kisha ikaja tuzo za KILLI
MUSIC je hao wasanii wawili tu ndio watakuwa wanashindana katika ubora kwa
Mwaka huo!!?? Huoni kama tumeziba Mianya ya wengine wengi wenye vipaji
kwasababu tulishawawekea mipaka Awali kutokana na Interest za Kibiashara!!? Sio
kama huu mfumo utaathiri mambo mengi sana!!??
HIP HOP
Katika Tasnia Ya Hip Hop pengine tokea atoke MSODOKI
Takribani miaka mitatu/miwili iliyopita, nahisi hatujapata zao lingine ambalo
Limefikia nafasi aliyokuwepo Msodoki!!! Tofauti na huku kwa wenzetu wanaoimba
tunaweza ona kuna mazao mengi kila siku!!
Haina maana kuwa hakuna vijana wanaofanya vizuri katika HIPHOP hapana, wapo wazuri sana lakini hawapati tu ile perfect PROMOTION!! Hilo ni Tatizo!! Muziki wa HipHop sidhani kama unapewa asilimia kubwa sana kwenye Promotions. Na sio sawa eti tuwe confortable kwasababu tu tunao wasanii watano tu wa HipHop ktk Mainstream!!
Haina maana kuwa hakuna vijana wanaofanya vizuri katika HIPHOP hapana, wapo wazuri sana lakini hawapati tu ile perfect PROMOTION!! Hilo ni Tatizo!! Muziki wa HipHop sidhani kama unapewa asilimia kubwa sana kwenye Promotions. Na sio sawa eti tuwe confortable kwasababu tu tunao wasanii watano tu wa HipHop ktk Mainstream!!
FINALLY
Wapo wasanii ambao watakuwa confortable kwasasa na hii situation na ni kwasababu tu Wana Silaha hivyo wanajiamini watashinda vita!!
Wapo wasanii ambao watakuwa confortable kwasasa na hii situation na ni kwasababu tu Wana Silaha hivyo wanajiamini watashinda vita!!
Ni wazo zuri sana lilikuwa na ipo siku tutalihitaji
katika soko letu lakini sio leo, ni kama alieleta wazo hili ametukurupusha!!
Kuna hasara nyingi kuliko faida tutakayopata!! Hata hiyo pesa tutakayopata kwa
mwaka kimakadirio ni ndogo sana tofauti na ukitoa wimbo kisha ukafanyiwa
promotions nzuri ukawa Hit kisha ukafanya Shows!! Otherwise tunaenda kuua shows
za pesa nyingi kwa pesa ndogo za mirabaha!!
Watazameni na wale ambao hawana silaha…wengine ndio
wametoka depo juzi tu hata hawajaiva…mkiwaingiza katika hii vita ni kuwajengea
makaburi mapema!!!
MAONI
Tuzibe gaps zingine kwanza katika sanaa yetu(zipo
nyingi na kuna vingi vya kurekebisha kabla hatujaanza na hili)Ni jambo Jema
kabisa hili lakini sio kwa hatua ya sanaa yetu ilipo sasa, tuanze na mengine!!
kisha tukishajiimarisha wote na silaha tukawa nazo wote basi utakuwa ni muda
wetu kuingia vitani!! Na tutashinda wote na
TUTASHANGILIA USHINDI WOTE!!
0 comments:
Post a Comment