skip to main |
skip to sidebar
PENZI LA SHISHI NA NUHU LAOTA MBAWA... SHISHI AFUTA TATTOO YA NUHU
Kuna taarifa mtaani kuwa penzi la mastaa wa muziki, Shilole na Nuh
Mziwanda limevunjika. Japokuwa sio mara ya kwanza kwa tetesi kama hizo
kuhusu couple hiyo, lakini safari hii kuna dalili kuwa inaweza kuwa
‘serious’.
Moja ya vitu vinavyoongeza nguvu ya tetesi hizo, Shishi amefuta ile
tattoo aliyochora kifuani kwake miezi kadhaa iliyopita, yenye jina la
‘Nuh’ na... kuchora UA juu yake.
Kipindi cha karibuni wawili hao hawaonekani pamoja kama ilivyozoeleka,
na kila mmoja amefuta picha zao za pamoja kwenye akaunti zao za
Instagram. Pia weekend iliyopita Shishi alifanya sherehe nyumbani kwake
ambayo hakusema sababu ya sherehe hiyo, lakini hakuwa na Nuh na wala
hakupenda kumzungumzia pale alipoulizwa na marafiki aliowaalika.
0 comments:
Post a Comment