Pages

Subscribe:

Saturday, September 3, 2016

KWETU YA RAYMOND YAZIDI KUFANYA VIZURI NJE YA TZ


14099337_1788426218082628_523354725_n
Muziki unasafiriki umbali usioweza kuufikiria. Na katika nyakati hizi za mchipuko mkubwa wa mitandao ya kijamii, kasi yake ni ya kutisha.  Lakini cha kupendeza zaidi, ni kuwa muziki huongea lugha ya dunia. Waweza kuupenda wimbo usiouelewa hata neno moja, lakini sauti na ala zake zikakufanya uusikilize bila kuuchoka. Lakini ni muziki uliotungwa kwa umaridhawa mkubwa unaoweza kukidhi viwango hivyo.

Kwetu wa Raymond ni mmoja wa nyimbo hizo. Sijui kama kijana huyu wa Mbeya aliyesota miaka mingi hadi kukaribia kukata tamaa na muziki, anajua kuwa ‘Kwetu’ ni dhahabu inayoendelea kupanda bei kila...
mshale wa saa unavyoyoyoma kwenda mbele kuhesabu dakika zinazopotea! 

Sidhani kama anajua kuwa zaidi ya nusu ya views milioni 3.4 ilizozikusanya video hii zimetoka nje ya Tanzania na Kenya ikiwa namba moja? Kuna uwezekano kuwa ni Wakenya wengi wameiangalia video hii kuliko hata watanzania wenyewe, anakotokea mchawi huyu wa mitindo huru katika rap – alaa ulikuwa hujui hilo?

Raymond ni msanii mkubwa wa baadaye wa calibre ya kimataifa ambayo ni wasanii wachache tu tunaowajua wa kuwezea kuifikia. Inashangaza mno katika umri huu mdogo kimuziki alionao kuweza kutengeneza kishindo kinachozifikia hata nchi zenye watu wasioelewa hata neno moja la Kiswahili.
Sijawahi kuona video yenye maoni chanya kwa zaidi ya asilimia zaidi 95 huku wachangiaji wengi wakiwa si Watanzania kama kwenye video ya kijana huyu.
Nenda kajionee mwenyewe na utaamini utabiri wangu kuwa, Ray ni kitu kikubwa cha baadaye Afrika.

0 comments:

Post a Comment