skip to main |
skip to sidebar
LULU AMPA MBWA WAKE JINA LA MTOTO WA DIAMOND
Video queen matata Bongo, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’ anadaiwa
kumdhalilisha mtoto wa Mbongo Fleva anayefanya vizuri kwa sasa, Nasibu
Abdul ‘Diamond’, Latifa ‘Tiffah’ kwa kumuita mbwa wake jina Shikiki,
ambalo pia ni jina jingine la...
utani la mtoto huyo.
Kwa mujibu wa chanzo chetu makini, mrembo huyo amemuita mbwa wake
huyo jina hilo, kitu ambacho kimetafsiriwa na wengi kama ni
kumdhalilisha mtoto huyo wa staa mkubwa Bongo.
“Jamani Diva anatafuta matatizo makubwa na D i a m o n d , kwanini
kampa mbwa wake jina kama hilo ambalo pia huwa linatumiwa na Tiffah? Ana
hatari sana,” kilisema chanzo chetu.
Gazeti hili lilipomtafuta Lulu na kumuuliza kuhusu ishu hiyo, alisema
ni kweli mbwa wake anaitwa Shikiki lakini hakuwa akijua kwamba mtoto wa
Diamond, jina lake lingine ni hilo.
“Jamani mimi sikuwa najua kabisa kama Tiffah, jina lake lingine ni
hilo, mimi nilimpa tu kama watu w e n g i n e wanavyowapa m a j i n a
mbwa wao,” alisema Diva.
0 comments:
Post a Comment