Sunday, November 20, 2016
BARNABA AWASHAURI WASANII WANAO UNGAUNGA KWENYE MUZIKI WATAFUTE KAZI NYINGINE
Hitmaker wa ‘Lover Boy’ Barnaba amewataka wasanii wanaofanya muziki kwa kubahatisha wabadilike au watafute kazi nyingine. Muimbaji huyo amekiambia kipindi cha Dj Show cha Radio One kuwa muziki unapoelekea kwa sasa ni mgumu na hakuna shabiki anayeweza kuongopewa kwa kuwa wanafahamu anafanya muziki mzuri na anayebahatisha.
“Wajitathimini wale wanaofanya muziki mzuri na muziki mbovu, wale wanaofanya muziki mzuri waongeze tu creativity. Wale wanaofanya muziki ambao hauishi nawashauri waache tu kwa sababu dunia...
tunayoenda hakuna ‘uongo uongo’ na mashabiki wanajua nani anafanya vizuri na nani anafanya vibaya na hakuna wakumdanganya utakuwa unajidanganya mwenyewe. Nashauri kila mtu aendelee kujituma hakuna uongo, hakuna mtu anayefanya uongo, hakuna mtu anayetaka kuongopewa,”amesema Barnaba.
Barnaba ameongeza kuwa wasanii waache kupoteza muda mwingi kwenye kutengeneza video pekee wafanye hivyo mpaka kwenye audio kuhakikisha zinakuwa nzuri pia.
Labels:
HABARI & UDAKU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment