Watu zaidi ya 96 wamefariki dunia na wengine zaidi ya 50 kujeruhiwa katika ajali ya treni Kaskazini mwa Jimbo la Uttar Pradesh nchini India.
Ajali
hiyo imetokea saa 6:30 usiku wa kuamkia leo kwa saa za Afrika Mashariki
ikihusisha treni ya mwendokasi ya Indore-Patna Express, ambapo takriban
mabehewa yake 14 yaliacha njia na kupinduka. Taarifa zinasema kuwa wengi walioathirika zaidi ni abiria katika
mabehewa mawili yalikuwa karibu na...
injini, ambayo yalipinduka kabisha na kusababisha miili ya airia hao kuharibika vibaya.
Kazi ya uokoaji inaendelea na huenda vifo vikaongezeka, huku askari zaidi ya 250 wakiwepo eneo la tukio.
injini, ambayo yalipinduka kabisha na kusababisha miili ya airia hao kuharibika vibaya.
Eneo la tukio
Abiria mmoja ambaye alikuwa katika behewa ambalo halijakumbwa na
kadhia hiyo, ameliambia Shirika la Habari ya Associated Press kuwa treni
hiyo ilikuwa ikienda kwa mwendo wa kawaida, lakini ghafla ilisimama na
kuanza tena mwendo, dakika chache kabla ya ajali kutokea.Kazi ya uokoaji inaendelea na huenda vifo vikaongezeka, huku askari zaidi ya 250 wakiwepo eneo la tukio.
Takwimu kwa mujibu wa BBC
0 comments:
Post a Comment