Pages

Subscribe:

Tuesday, November 1, 2016

HII NDIYO KAULI YA BARNABA BAADA YA MH. NAPE KUMTEMBELEA KTK STUDIO YAKE


Image result for BARNABA
“Dont Call me Lover Boy” Barnaba anakwambia hivyo katika ngoma yake ya “Lover boy” inayofanya vizuri kwasasa, Barnaba ameamua kutufungukia ujio wa Mh.Nape Nauye katika studio yake.

Kama utakumbuka vizuri kabisa mwezi uliopita Barnaba alifanyiwa ziara ya ghafla lakini sio ya kutumbuliwa jipu kama wengi ambavyo tumezoea, alifanyiwa...
ziara ya waziri wa Habari Nape Nnauye na wakazungumza mambo mengi sana yanayo husu kitaifa na kijamii.
Akiongea Barnaba alisema kwamba Nnape Nauye alikuja ofisini kwake kama mtu ambaye wanafaamiana kwa muda mrefu katika tasnia ya muziki wa bongo fleva, kikubwa ambacho kilichofanya ujio wa Nape Nnauye ni kuja kutupa ushauri na vilevile kutembelea studio ya Barnaba kwasababu alisikia kwamba Barnaba amefungua studio, kingine kikubwa pia alikuwa amemletea kazi ambazo zilipaswa kufanywa na Barnaba.

0 comments:

Post a Comment