Pages

Subscribe:

Tuesday, November 1, 2016

MATONYA: KUNA WATU WAMEKUJA KUHARIBU MUZIKI WETU WA BONGO FLEVA

12224097_927597553975092_1780800703_n
Msanii mkongwe wa muziki, Matonya amewataka wadau mbalimbali wa muziki kuwa makini na watu ambao wamekuja kuuharibu muziki wa bongofleva, Muimbaji huyo ambaye amewahi kufanya vizuri na wimbo ‘Vaileti’ na nyingine nyingi, ameiambia Bongo5 kuwa kuna vijana wameingia kwenye muziki bila kuwa navipaji.

“Mimi napenda kuwapongeza wasanii wote wazuri ambao wanafanya vizuri lakini kuna watu pia hawastahili kupongezwa kwa sababu...
wamekuja kuuharibu muziki wetu,” alisema Matonya. “Kwahiyo wanaokuja kwa matusi kwa nia ya kuuharibu muziki tutawachukia sana,” Aliongeza,“Kuna watu wamekuja kuuharibu muziki wa bongofleva. 

Kwa sababu tunaona kabisa kuna watu ambao walikuwa hawana ajira wamepata ajira. Sisi ambao tumefanya muziki huu kwa muda mrefu tumeona mafanikio pamoja na connection. Lakini kuna watu ambao hawajiwezi wanakuja na wanafanikiwa kwenye muziki, kwahiyo tukiwaruhusu kuuharibu muziki wetu kwa njia yoyote watakuwa wameharibu chakula cha watu wengi,”
Pia muimbaji huyo wiki hii ameachia wimbo mpya ‘Mr Legeza Kidogo’ wa wasanii wa kundi lake jipya liitwao ‘Black Image’.

0 comments:

Post a Comment