Pages

Subscribe:

Thursday, November 10, 2016

TAARIFA YA WEUSI KUFANYA KAZI NA DOGO JANJA UKWELI UKO HAPA


Ni baada ya kufanya bonge la show pande za Leaders Club kwenye Fiesta pale ambapo Dogo Janja alipanda jukwaani wakati kundi la Weusi wakiwa wanaperform na kwenda kucover part ya rapper A.K.A wa South Africa kwenye collabo ya Don’t Bother yakwake Joh Makini.

Ndipo baada ya tukio hilo rapper Nikki wa Pili wa kundi la Weusi alichukua nafasi ya kummwagia sifa kibao rapper Dogo Janja na kuweka wazi kwamba yeye...
anamchukulia kama msanii wake bora kwa mwaka huu.

Kwenye ukurasa wake wa insta Nikki aliandika:
Abduli kachaa AkA @dogojanjatz ....kijana mdogo aliyefaulu kwa max za juu somo lililoshinda mamilioni ya watu, wasomi, wafanyabiashara, wanamichezo..watu wa rika zote......somo la kuanguka na kuinuka katika ubora wa kiwango cha juu, nidhamu, kufuta makosa yote.........show zake sasa zinaacha history, brand yake iko na professional look, confidence iliyovuka mipaka.....kwa umri wake na aliyo ya fanya 2016...namtangaza kuwa msanii wangu bora 2016...... 


Ndipo baada ya matukio hayo mawili maswali yakaja mengi katika vichwa vya wapenzi wa burudani na kuhisi kuwa huwenda kuna mpango wowote wa kundi la Weusi kufanya kazi na Dogo Janja.
Perfect255 imepiga story na msemaji wa kundi la Weusi Nikki wa Pili na kumuuliza ni michongo gani wamepanga kuhusu kufanya kazi na rapper Dogo Janja.
“Weusi ni kampuni na inaweza kufanya biashara na mtu yeyote, kwahiyo kama Dogo Janja yeye atahitaji kufanya biashara na Weusi sisi tuko tayari kufanya nae biashara lakini sio kama kujiunga nae kama kundi kwasababu sisi sio kundi sisi ni kampuni.”
Hayo ni baadhi ya maneno ambayo aliyazungumza Nikki wa Pili wakati akitolea ufafanuzi issue ya Dogo Janja. Play hii video hapa chini kumsikiliza mwanzo mwisho mwenyewe akizungumza.

0 comments:

Post a Comment