Shirika la afya duniani yaani who linatoa taarifa kwamba kila mwaka
zaidi ya watu milioni moja hujiua kwa sababu mbalimbali... nchini
marekani ni chanzo cha tatu cha vifo cha vijana kati ya miaka 15 mpaka
24 na ni chanzo cha 11 cha vifo kwa watu wote nchini humo.
kimsingi kujiua sio ugonjwa wa akili lakini ni matokeo ya msongo wa
mawazo na magonjwa ya akili yanayosababishwa na matatizo mbalimbali ya
kiafya, kiuchumi, kimahusiano, msongo wa mawazo, matumizi ya dawa fulani
za kulevya,kukoza kazi na kufiwa na wapendwa wetu.
taarifa hiyo inaongeza kua watu wenye umri wa miaka 15 mpaka 44 hujiua
zaidi kuliko makundi yote ya umri, wanaume huongoza kwa kujiua kuliko
wanawake lakini... wanawake huongoza kwa kujaribu kujiua kuliko wanaume.
vijana ndio moja ya kundi kubwa ambalo haliwezi kuvumilia matatizo ya
kimaisha yaani mtu akiachwa na mpenzi, akikosa kazi, akifilisika,
akigunduliwa na ugonjwa hatari kama ukimwi, kansa au kisukari basi haoni
sababu za kuendelea kuishi.
kwa miaka 45 iliyopita tatizo la kujiua limeongezeka kwa 60% na kwa sasa
kila baada ya sekunde 40 mtu mmoja hujiua, na inakadiriwa kwamba mpaka
mwaka 2020 kila baada ya sekunde 20 mtu mmoja atajiua, baadhi ya data za
kujiua hukosekana sababu ya watu kuonekana wamepotea kumbe wamejiua na
miili yao haikupatikana.
tatizo la kujiua au kujaribu kujiua nchini tanzania pia ni kubwa sana
kuliko linavyofikiriwa kulingana na kukosekana kwa huduma za ushauri
hasa kwa watu wenye shida zinazotaka ushauri wa kina na pia kuhisi watu
hawa wamekufa ghafla kulingana na njia walizotumia kujiua.
makundi gani wako kwenye hatari ya kujiua?
- wazee ambao wamepoteza mme au mke kwa vifo au talaka.
- watu ambao wamejaribu kujiua kipindi cha nyuma
- watu ambao kuna historia za kujiua kwenye ukoo wao
- watu wenye historia ya kuumizwa kihisia au kulazimishwa kingono
- watu ambao hawajaolewa au kuoa, hawana ujuzi au hawana kazi
- watu wanaotumia madawa ya kulevya
- watu ambao ni wakorofi sana kwenye jamii
- watu waliowahi kuugua magonjwa ya akili.
katika mazingira yetu watu hushtuka kusikia fulani kajiua lakini
ukifuatilia kwa makini mtu huyu alionyesha dalili zote za kutaka kujiua
lakini watu hawakuzitambua na dalili hizo ni kama ifuatavyo.
kukosa raha kwa muda mrefu; mtu anakaa miezi sita mpaka mwaka
akiwa hana raha huku akilalamikia jambo moja ambalo linamsumbua, kwa
kawaida binadamu tuna matatizo mengi lakini mtu kuganda na tatizo moja
kwa muda mrefu na kukosa msaada basi ujue anaelekea kubaya.
kua mpole ghafla; mtu ambaye kwa muda mrefu amekua akililia jambo
fulani bila msaada kisha akakaa kimya ghafla na kuonekana kawaida na
wakati jambo lililokua linamkwaza bado halijapata suluhisho huenda
amejkata shauri sasa anajiua.
kukosa tumaini la siku zijazo; huenda huenda mtu ana madeni
makubwa ya kifedha, biashara yake imekufa, amekutwa na ugonjwa hatari,
kafiwa na wazazi, mume,mke au watoto na vitu hivyo vilikua nguzo yake
kuu na haoni tena maisha yake ya baadae..
kujitenga na watu; mtu anaanza kujitenga na ndugu, jamaa na
marafiki yaani anapenda kukaa peke yake bila kujichanganya na watu na
hata mambo aliyokua akiyapenda kuyafanya zamani katika sehemu za starehe
sasa hana raha tena akiyafanya.
kukosa usingizi; mtu anayeelekea kujiua hukosa usingizi kutokana
na matatizo yanayomkabili, usku mzima hua macho na kitu kidogo kikipita
nje lazima atakisikia...muda huu huwaza na kuwazua kuhusu matatizo yake
ambayo kwa muda mrefu sasa yamekosa suluhisho na yeye haoni sababu ya
kuendelea kuishi.
kubadilika ghafla kimtazamo; mtu aliyekua mchangamfu ghafla
anakua mpole, mtu aliyekua mtanashati ghafla anaanza kuvaa hovyo na
kutembea kwa haraka sana huku akiongea peke yake, vitu vya kawaida sasa
vinamchukiza na kua mkali kwa chochote anachoambiwa.
kutishia kujiua; zaidi ya 75% ya watu wanaotaka kujiua watatoa
vitisho kwamba siku moja nitajiua, katika hali ya kawaida mtu unaweza
ukapuuza ukidhani ni masihara lakini nakwambia ukioana mtu anatishia
kujiua basi usipuuze kauli zake kitaalamu inaitwa 'call for help' kwamba
anaomba msaada ili asijiue na hii ndio dalili kuu muhimu kuliko zote.
kuanza kujiaandaa; mtu anayetaka kujiua ataanza maandalizi kwa
kugawa baadhi ya mali zake, kuwatembelea ndugu na jamaa, kuandika usia
wa mali zake, kuandika barua ya chanzo cha yeye kujiua, na huweza kunua
vitu vya kujiua kama dawa, sumu, bunduki au kamba.
je kujiua kunaweza kuzuilika?
ndio mtu anayetaka kujiua mara nyingi anakua anataka msaada, jaribu
kukaa na kumuuliza kitu gani kinamsumbua na kama amefikiria kujiua..
mshauri kwamba matatizo hayapo kwa ajili yake tu kwani kuna watu wengi
wenye matatizo zaidi yake na kikubwa ni kuvumilia kipindi hiki kigumu
lakini pia msaidie kwenda hospitali au kituo chochote akaonane na
mshauri, kama una nafasi ya kumsaidia basi msaidie kulingana na tatizo
lake..
nifanye nini kumsaidia mtu anayetaka kujiua?
ukishagundua mtu anataka kujiua kuna mambo ya msingi sana unatakiwa kuyafanya ili kumsaidia asijiue kama ifuatavyo.
usimuache peke yake; hakikisha unakaa naye muda wote na ikiwezekana piga simu kwa ndugu na jamaa na marafiki ili wakusaidie.
weka mbali vitu vya hatari; kama kuna kamba, au silaha yeyote
basi ficha mbali lakini pia mwambie muhusika kwamba kama kuna kitu
chochote ameshenunua kujidhuru basi mwambie akukabidhi uviweke mbali,
wasiliana na daktari ; kama ni mgonjwa wa akili ambaye
anafahamika siku nyingi basi mpigie simu daktari wake ili aweze
kurudishwa hospitali na kulazwa kabisa na kama hua sio mgonjwa wa akili
basi apelekwe hospitali kwa uchunguzi zaidi.
mwisho; huenda wewe msomaji ndio muhusika ambaye umekata tamaa na
unataka kujiua, nikupe moyo kwamba matatizo hayakuumbwa kwa ajili yako
tu...kuna watu wengi wana matatizo makubwa zaidi yako na wengine
waliwahi kua kwenye matatizo kama hayo na sasa wana mafanikio
makubwa..usijiue hata kama umepata aibu au tatizo kubwa kiasi gani
maishani mwako.
kama ni mpenzi utapata mwingine, kama ni mtaji utapata
mwingine, kama ni ugonjwa wewe sio wa kwanza kuugua hivyo jifunze
kupambana nao...kumbuka muda ndio daktari mkuu yaani wazungu wanasema
time will heal you.
0 comments:
Post a Comment