Zipo pilipili za kuwasha kama pilipili mbuzi na pilipili kichaa lakini pia zipo ambazo haziwashi kama pilipili hoho, hivyo kama wewe ni muoga wa pilipili za kuwasha basi kula hata pilipili hoho ili ufaidike na...
faida nyingi sana zinazopatikana kwenye vyakula hivyo. zifuatazo na faida muhimu zinazopatikana kwenye pilipili.
kiasi kikubwa cha vitamin c; utafiti umeonyesha kwamba pilipili
zina kiasi kikubwa cha vitamin c kuliko hata kile kinachopatikana kwenye
matunda kama machungwa na machenza, vitamin c ni nzuri kwa kinga ya
mwili, na kulainisha ngozi.
husaidia kupunguza uzito; pilipili huongeza kasi ya mwili kufanya
kazi na kuchoma mafuta[metabolism], kemikali ya piperin iliyoko kwenye
pilipili huzuia mwili kutengeneza mafuta mapya, lakini pia zenyewe
zikiwa na ujazo mdogo wa ndani kiasi kwamba hata ule nyingi kiasi gani
haziwezi kukuongeza uzito, kumbuka pilipili unazowezakula nyingi ni zile
ambazo haziwashi.
huzuia magonjwa yasiambukizwa; kemikali ya capsaicin
inayopatikana kwenye pilipili hupunguza lehemu mwilini au cholestrol,
husaidia kupunguza sukari kwa wagonjwa wa kisukari na kupunguza maumivu
ya mwili.
huzuia kansa mbalimbali; kiasi cha sulfur kinachopatikana kwenye
pilipili kimethibitika kua vizuri sana katika mchakato wa kuzuia kansa
za mbalimbali za mwili.
hukinga mishipa ya fahamu; pilipili za aina mbalimbali hua na
vitamin b6 ambayo ni muhimu sana katika afya ya mishipa ya fahamu,
ukosefu wa vitamin hii ni moja ya vyanzo vikuu vya kupata ngazi mwilini
na kuhisi dalili za kuwaka moto.
hutunza macho; lutein ni enzyme inayopatikana kwenye pilipili,
katika umri mkubwa wa maisha hufanya kazi ya kuzuia kutokea kwa mtoto wa
jicho[cataract],huu ni weupe unaotokea kwenye lens ya jicho na kumfanya
mtu apate upofu.
hupunguza kasi ya uzee; kiasi kikubwa cha vitamin e kilichopo
kwenye pilipili hulainisha ngozi sana na kumfanya mtumiaji kuonekana
kijana na mwenye nguvu hata katika umri mkubwa wa maisha.
huongeza virutubisho mwilini; ikipikwa na moto kidogo bila kuiva sana, pilipili ina virutubisho vingi muhimu kwa ajili ya afya ya binadamu.
hutibu mafua; mgonjwa mwenye mafua yaliyoziba kabisa akila
pilipili kamasi zote zilizoganda hugeuka na kua laini sana na kumpa
nafuu ya upumuaji.
husaidia mmeng'enyo wa chakula; pilipili husaida mwili
kutengeneza kiasi kikubwa cha kemikali ya hydrochloric acid
inayopatikana tumboni ambayo kazi yake ni kuongeza mmeng'enyo wa chakula
hivyo kuupa mwili virutubisho vyote muhimu.
0 comments:
Post a Comment