skip to main |
skip to sidebar
AUNT LULU ATOA OFA YA PENZI KWA PAPII KOCHA KISA MWONEKANO
Mwanadada aliyewahi kuwa mtangazaji
ambaye haishiwi na matukio, Lulu Semagongo ‘Aunt Lulu’ amesema kuwa yupo
tayari kumpa ofa ya mapenzi mwanamuziki Johnson Nguza ‘Papii Kocha’
mpaka asahau maisha aliyopitia.
Akiongea Aunt Lulu
alisema amemuona Papii amekuwa mpya na anapendeza kila kukicha hivyo
amejitolea kumpatia penzi iwapo atamkubalia ili...
asahau kabisa shida za
dunia.
“Unajua mimi najua kupenda, iwapo
nitampatia penzi Papii mbona atasahau kabisa alipotoka, yeye akubali tu
maana sijawahi kuona mahusiano yake, naamini kwa kipindi alichokaa jela
kama angekuwepo mwanamke angejitokeza lakini haijawa hivyo, mimi nipo
kwa ajili yake,” alisema Lulu.
Mwandishi wetu alijaribu kumpigia simu Papii ili kumfahamisha juu ya ofa hiyo ya mapenzi lakini hakuweza kupatikana mara moja.
Source: Global publishers
0 comments:
Post a Comment