Muigizaji mkongwe wa Bongo movie Aunty Ezekiel amesemekana kuwa
matatizoni na mpenzi wake Moses Iyobo ambaye ni mcheza shoo/ dancer wa
Msanii wa Bongo fleva Diamond Platnumz.
Aunty Ezekiel na Mose Iyobo wamezaa pamoja mtoto mmoja wa like
anayeitwa Cookie, mwanzoni wakati mahusiano yao yanaanza wapo watu wengi
sana ambao waliponda kwa kudai kuwa Aunty hana hadhi ya kuwa na mtu
kama Iyobo ambaye ni mcheza shoo lakini...
wenyewe walipendana na walilidhihirisha hilo.
Aunty na Iyobo ni moja kati ya couple chache Bongo za mastaa ambazo
hawana sana skendo mtandaoni au hawana sana kiki lakini kuna mara chache
ambazo Aunty alitumia mitandao ya kijamii kulalama kuhusiana na
uhusiano wake na Iyobo.
Miezi michache iliyopita Aunty Ezekiel alitumia ukurasa wake wa
Instagram kumlalamikia mwanamke amnaye alikuwa anajigonga kwa Mose Iyobo
na alifunguka nakudai kuwa mwanamke huyo alikuwa amedhamiria kumharibia
familia yake.
Tangu hapo kumekuwa na tetesi kuwa penzi la Aunty na Iyobo limekuwa
likilega lega ingawa hakuna hata mmoj kati yao aliyethibitisha tuhuma
hizo.
Siku ya Jana Aunty aliandika maneno yaliyowapelekea watu wengi
kudhani kuwa labda ni kweli penzi lake na baba watoto wake Moses Iyobo
liko matatani. Kupitia ukurasa wake wa Instagram aliweka picha
inayomuonesha akiwa na mawazo makali alafu akaisindikiza kwa maneno
yafuatayo:
Sina kawaida ya kuweka maisha yangu kwenye mitandao ya kijamii ila huku tunakoenda dah! Wanaume?”.
Maneno hayo ndio yalizidi kuzua tetesi kuwa labda penzi la Aunty na
Iyobo limekufa kwa maana ni juzi tu Iyobo aliandika kwenye ukurasa wake
wa Instagram kuwa anatamani kungekuwa sehemu ya wakina baba kudai haki
zao wakinyimwa unyumba maana amenyimwa unyumba na Aunty!.
0 comments:
Post a Comment