Msanii
Zuwena Mohamed alimaarufu kama Shilole amekaidi adhabu aliyopewa na
Baraza la Sanaa Tanzania (Basata) iliyomtaka kutoshiriki masuala ya
sanaa ndani na nje ya nchi kwa mwaka mzima.
Shilole
amekaidi adhabu hiyo baada ya kuonekana akifanya show katika kampeni za
Chama Cha Mapinduzi (CCM) akimnadi Mgombea nafasi ya urais wa chama
hicho Dk. John Magufuli wakati wapo jijini...
Mbeya siku kadha zilizopita.
Mbeya siku kadha zilizopita.
Kipindi
cha Planet Bongo kilitaka kufahamu endapo adhabu ya msanii huyo
imefutwa, na kuwatafuta Baraza la Sanaa Tanzania ndipo hapo Mama Sharua
ambaye yupo katika Idara ya kukuza Sanaa na Masoko alipokanusha kufutwa
kwa adhabu ya msanii huyo na kusema adhabu yake ipo palepale na kama
amefanya shoo amekaidi adhabu hiyo.
"Shilole
anatambua wazi kuwa anaadhabu hiyo hivyo kama amefanya shoo sisi kama
Basata itabidi tukae chini na kufuatilia juu ya suala hilo na tukigundua
kuwa kuna ukweli sheria itachukua mkondo wake," alisema Mama Sharua.
Basata
imesema kitendo alichofanya msanii huyo ni wazi kuwa ameshindwa
kuheshimu adhabu iliyotolewa na hivyo lazima sheria ichukue mkondo wake
kwani hakuna mtu ambaye yupo juu ya sheria.
Planet
Bongo ilimtafuta msanii Shilole kutaka kufahamu kwanini ameamua kufanya
maamuzi hayo ili hali anatambua kuwa anaadhabu ambayo inamkabili ndipo
hapo msanii huyo aliposema kuwa tuyaache hayo mambo kwani ni mambo ya
kiserikali zaidi.
0 comments:
Post a Comment