Wednesday, September 2, 2015
STORY: PETE YA JINI SABRAH... EPISODE 4 To 7
PETE YA JINI SABRAH - 4 To 7
Mtunzi : Mwinyimvua
0789 569355
Gafla baba sophia roho iliacha mwili sikuweza kuamini kuona kitendo kile kutokea mikononi mwangu machozi yalini tiririka mashavuni kwangu huku fredy na mama sophia pasipo kujua nini kinaendelea " Fredy Fredy simamisha gari " nilisikika nikisema " Kuna nini?? " Sauti ya fredy ilisikika huku akipunguza mwendo wa gari " Jamani fanyani haraka mume wangu nitamkosa...
" Sauti ya mama sophia ilisikika pia huku muda wote akilia kwa hali haliyokuwa naye mumewe baba sophia Fredy alipunguza mwendo hatimaye buguruni marapa akasimamisha gari huku akigeuka upande wa nyuma nilipokuwa mimi na mwili wa baba sophia ambaye alifariki muda tu " Kuna nini saidi?? "
Fredy aliuliza " Baba sophia hatunaye duniani " Nilimjibu fredy kwa sauti ya chini huku mimi nikiwa nimeu kumbatia mwili wa marehemu " Nini oooooh!! my god " sauti ya Fredy ilisikika huku akionekana mtu alieyeishiwa nguvu na kulalia usukani wa gari Mama sophia hakuweza kuamini kauli zilizokuwa zikisikika muda ule juu ya kifo cha mumewe Nae nilimuona gafla akizimia mule mule garini.
kiza muda ule kilichukua nafasi yake hakika niliogopa sana muda ule niliangalia saa pale mbele ya gari ilikuwa saa 9 : 20 Mara nilimuona fredy aki inuka taratibu pale kwa usukani huku macho yake yakiwa yame badilika rangi uso wake ulitapakaa machozi juu ya tukio lililotutokea " Sasa tufanyaje saidi?? " Fredy aliniuliza " Mimi nakusikiliza wewe ndugu yangu " Nilimjibu fredy " Itabidi tugeuze safari ''.
EPISODE 5
Fredy alisema huku akigeuza gari kuelekea tulipotoka " Fredy mbona unarudi tulipotoka ?? " Mimi nilisikika nikimu uliza Fredy huku mwili wa marehemu baba sophia ukiwa mikononi mwangu " Saidi rafiki yangu bora mwili tu upeleke nyumbani kwa marehemu muda huu kuliko ku upeleka hospitali " " Kwanini unasema hivyo Fredy?? "
Nilisikika nikimuuliza fredy Kipindi chote wakati nikizungumza na fredy mama sophia alionekana kutopata fahamu baada ya kuzimia pale alipogundua mumewe baba sophia amefariki " Saidi rafiki yangu mimi nimeona mbali ndo maana na kwambia hivyo " Fredy alisikika akisema haikuchukua muda mrefu tulifika nyumbani huku kiza kikiwa bado kina tawala usiku ule nakumbuka ilikuwa kama saa 10 : 30.
Taratibu tuliutoa mwili wa baba sophia ku upeleka ndani kwake huku mama sophia akionekana bado kutopata fahamu Tuli mbeba pia mama sophia kumpeleka ndani " Saidi Saidi chukua simu ya mama sophia uwa pigie ndugu zake " Fredy alisikika akisema " Sawa " Nilimjibu fredy huku nikielekea chumbani kitandani alipolala mama sophia Taratibu nilimpapasa mama sophia mifukoni mwake hakika mama sophia alikuwa na umbo la kipekee.
Miguu alija aliwa kifua ndo usiseme hatimaye niliipata simu ya mama sophia niljaribu kuangalia majina kadhaa kwenye simu yake hatimaye nikaliona jina la dada yake mama sophia aitwaye mama zainabu..
EPISODE 6
Nilijaribu kumpigia simu yake iliita bila kupokelewa nilijaribu mara kadhaa kupiga ile namba tena kipindi chote icho wakati mimi nipo chumbani fredy na mkewe walionekana nje wakiwa katika hali ya kuto amini juu ya msiba wa baba sophia " Hallow!! Hallow!! mama sophia " Sauti ya mama zainabu ilisikika kwenye simu " Hallow!!
Wewe mama zainabu dada yake mama sophia? " Nilisikika nikimu uliza swali " Ndi...ndi...ndio " Sauti ya mama zainabu ilisikika huku ikionekana yenye kigugumizi. " Mimi naitwa saidi ni jirani wa mama sophia naomba uwape taharifa ndugu wengine huku shemeji yenu baba sophia amefariki " Sauti yangu ilisikika Muda ulizidi kujongea hatimaye kuka pambazuka mbingu ilionekana yenye kujaa tabasamu huku ndege mbalimbali wakionekana kuelea hewani.
Watu wengi majirani walishikwa na butwaa asubuhi ile juu ya kifo cha baba sophia ndugu wa mama sophia na baba sophia walionekana pia wakionekana wenye majonzi mazito " Mume wangu!! Mume wangu!! umeni acha peke yangu " Sauti ya mama sophia ilisikika ikilia kwa uchungu ikitokea ndani vilio vilisikika viki tawala eneo lile huku ma swali kadhaa yakiwa vichwani mwa watu juu ya chanzo cha kifo cha baba sophia.
" Pole sana kijana " Sauti laini ya kike ilisikika ikiniambia " Ahsante " Nilimjibu yule mtu ingawa sikumjua vizuri kiundani " Unani fahamu mimi?? " Yule mwana mke alini uliza " Hapana " Nilimjibu " Usijali utanijua tu " Sauti ya mwana mke yule...
EPISODE 7
Sauti ya mwana mke yule ilisikika huku akitokomea kusiko julikana maswali kadhaa yalinijia kichwani pasipo kupata majibu yeyote juu ya mwana mke yule vilio viliendelea kusikika muda wote eneo lile hatimaye ndugu wa marehemu baba sophia waka amua ndugu yao akazikwe kijijini kwao MZENGA huko ndipo baba yake marehemu baba sophia ndipo alipozikiwa " Saidi saidi njoo upesi " Sauti ya fredy ilisikika ikiniita taratibu nilijongea hadi kwa fredy " vipi kaka??
" Nilimu uliza fredy " Familia ya marehemu baba sophia imetuteua tukazike " Fredy alisema " Sawa kaka itabidi iwe hivyo " nilimjibu fredy gafla mwili wangu nikahisi una mabadiliko flani yasiyo kuwa ya kawaida nili hisi baridi kali katika mwili wangu ingawa hali ya hewa siku hiyo haikuwa ya mvua jua liliwaka muda wote miguu ilianza kuwa na ganzi nilishindwa kusimama muda ule pale nilipo simama huku vilio viki endelea kusikika.
mwili wa baba sophia uliingizwa kwenye gari taratibu tayari kwa safari ya kwenda kumu hifadhi katika nyumba yake ya milele majirani walijongea taratibu kum sindikiza marehemu baba sophia " Saidi saidi njoo upande gari twende " sauti ya fredy ilisikika kwa mbaali huku yeye akiwa tayari kesha panda tayari kwa safari " Nakuja kaka " nilimjibu fredy huku mwili wangu ukiwa katika hali ile ile ya awali.
Nilijongea taratibu kupanda ile gari cha kushangaza yule mwana mke nilimuona tena akiwa kapanda kwenye ile gari ya maiti nili jaribu kutaka kumu uliza fredy cha ajabu ulimi wangu ulikuwa mzito nilibaki pale chini niki shikwa na butwaa nisijue hata cha kufanya " Saidi rafiki yangu vipi " sauti ya fredy ilisikika huku akinipa mkono nipande kwenye gari la maiti chaku shangaza wakati napanda kwenye ile gari ya maiti yule mwana mke hata siku muona!!
Hali ile ilinitisha sana " Fredy humu kwenye gari ujamuona mwana mke kavaa IJABU ?? " nilisikika nikimu uliza fredy " Mwana mke??? " Fredy nae aliniu liza " Ndio " nilimjibu fredy Wakati nikiendelea kujibizana na fredy gafla...... ITA ENDELEA
Labels:
LOVE & STORY
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment