Pages

Subscribe:

Saturday, February 13, 2016

HISTORIA YA YANGA KTK MICHUANO YA KLABU AFRIKA

Historia ya Yanga katika michuano ya Klabu Afrika
Yanga imekuwa ikijizolea sifa kubwa kwa kila mwaka kushiriki michuano ya kimataifa kama siyo hiyo ya Ligi ya mabingwa basi itakuwa ile ya Kombe la Shirikisho lakini imekuwa haifiki. Wawakilishi wa Tanzania bara katika michuano ya Ligi ya mabingwa Afrika Yanga kesho wanatupa karata yao ya kwanza kwa kupambana na Cercle de Joachim ya Mauritius.

Yanga inapewa nafasi kubwa ya kushinda na kusonga mbele hatua inayofuata kutokana na kiwango bora ilichokuwa nacho hivi sasa lakini pia kuwa juu kwa kiwango cha...
soka ukilinganisha na Mauritius ambayo kwa sasa inapambana kutoka katika soka la ridhaa kuja la biashara.

Kitu kingine kinachoifanya Yanga kupewa nafasi ya kushinda na ubora wa kikosi ilichonacho ambacho kinaundwa na nyota kutoka mataifa saba tofauti ambayo ni Togo, Niger,DR Congo, Rwanda,Zimbabwe  Burundi na Tanzania huku wapinzani wao Cercle de Joachim, asilimia kubwa wakiwa ni wazawa wa Mauritius.

Mbali na kuwa na nyota kutoka mataifa hayo saba lakini hata gharama ya usajili iliyotumika inatofauti kubwa na ile ya wenyeji wao Cercle de Joachim ambapo hata mshahara wa mchezaji mmoja mmoja hawalingani na wanyeji wao
Pamoja na hayo Yanga imekuwa ikijizolea sifa kubwa kwa kila mwaka kushiriki michuano ya kimataifa kama siyo hiyo ya Ligi ya mabingwa basi itakuwa ile ya Kombe la Shirikisho lakini imekuwa haifiki mbali.

Mwaka huu ni wa 24 kushiriki ligi ya mabingwa Afrika lakini haijawahi kufika mbali zaidi ya kutolewa katika raundi ya awali au ya kwanza ikizidi sana raundi ya pili na hasa inapokutana na timu kutoka Kaskazini na Magharibi.
Wababe hao wa kihistoria kwa kubeba ubingwa Ligi ya Vodacom mara 25, wamekuwa wakizinyanyasa sana timu ndogo wanazopangiwa nazo hatua ya awali za kutoka Comoro Botswana au Zimbabwe lakini breki yao inapofikia kupambana na wababe hao wa Afrika.

Kabla ya fainali za mwaka huu mara ya mwisho timu hiyo kushiriki ligi ya mabingwa Afrika ilikuwa ni mwaka juzi ambapo timu hiyo ilitolewa na National Al Ahly kwa changamoto ya mikwaju ya penalt baada ya kutoka sare ya kufunga mabao 1-1 Yanga wakishinda bao 1-0 nyumbani na katika mchezo wa marudiano Ahl nao wakashinda 1-0 na kuamuriwa zipigwe penati.

Kabla ya hapo Yanga iliitoa Komorizone ya Comoro, kwa idadi kubwa ya mabao kiasi cha kumfanya winga mrisho Ngasa kuwa mfungaji bora wa michuano hiyo kwa kufunga Hart trick mbili katika michezo yote miwli ya nyumbani na ugenini.
Baada ya hapo msimu uliofuata Yanga ilikosa ubingwa ikamaliza msimu nafasi ya pili ambapo ilishiriki michuano ya kombe la Shirikisho mwaka jana na safari hii ilionekana kujipanga kiasi kwa kufika hadi raundi ya tatu kabla ya kutolewa na Etoile du Sahel kwa mabao 2-1.

Yanga ilianza vizuri kwa kuwatoa BDF, XI ya Botswana baada ya hapo ikapangiwa FC Platinum ya Zimbabwe lakini ilipokutana na Etoile mambo yakawa magumu endapo ilionyesha kila dalili kama ingekaza ingefanikiwa kucheza hatua ya makundi kama ilivyofanya mwaka 1997 lakini ilifungwa bao 1-0 katika mchezo wa marodiano na kuondoshwa kwenye michuano hiyo.

Rekodi hiyo fupi inaonyesha namna klabu za Tanzania hasa Simba na Yanga zinapofeli hasa zinapokutana na timu za ukanda huo jambo ambalo linatakiwa lifaniwe kazi ili ziweze kuvunja miiko hiyo kama ilivyofanikiwa TP Mazembe, kutoka ukandaa wa Afrika Mashariki na Kati.

Pamoja na umaarufu mkubwa iliyonao klabu ya Yanga haina kitu kikubwa cha kujivunia Afrika zaidi ya rekodi hiyo ya kucheza hatua ya makundi na kumaliza kwa aibu kwani iliweza kufungwa mabao sita na Maning Rangers ya Afrika Kusini.
Mwaka 2012 Yanga ilikuwa bingwa wa Tanzania na kushiriki michuano ya Ligi ya mabingwa safari hiyo iliaga mapema michuano hiyo kwani mchezo wa raundi ya kwanza ilipangiwa Zamalek ya Misri na haikuweza kufa dafu baada ya kutupwa nje kwa jumla ya mabao 2-1.

Matokeo hayo mabaya kwa timu za Tanzania hayapo kwa Yanga bali hata klabu nyingi ne kama Simba na timu ya Taifa ‘Taifa Star’ ingawa Simba yenyewe iliweza kuonyesha jeuri kwa kujitutumua kwa kucheza fainali ya kombe la CAF, mwaka 1993 na kufungwa mabao 2-0 uwanja wa taifa hiyo ikiwa ni baada ya kutoka sare ya bila kufungana Abdjan Ivory Coast na Stella Artoia.

Mbali na hapo mwaka 2003, Simba iliweka rekodi ya kuwavua ubingwa wa Afrika Zamalek, baada ya kutokanao sare ya 1-1, Simba wakianza kupata ushindi wa bao 1-0 uwanja wa Uhuru Dar es Salaam na Zamalek kusawazisha katika mechi ya marudiano iliyopigwa Cairo Misri na Simba kufanikiwa kutinga hatua ya makundi ingawa haikufanikiwa kusonga mbele.

Kwa mwenendo huo ni wazi timu za Tanzania zinapaswa kufanya usajili mzuri wa wachezaji wakizingatia ushiriki wao wa michuano hiyo mikubwa ya Afrika ili ziweze kufanya vizuri kama ilivyo kwa TP Mazembe na nyingine za Afrika Magharibi.

0 comments:

Post a Comment