skip to main |
skip to sidebar
PESA ALIZOVUNA MR NICE MIAKA YA NYUMA ZAANZA KUFANYA KAZI
Msanii
mkongwe na mwanzilishi ya style ya TAKEU, Mr Nice amefunguka kwa kusema
kuwa bado yupo vizuri kiuchumi tofauti na watu wanavyodhani kwamba
amefilisika.
Akizungumza
na Bongo5 Alhamisi hii, Mr Nice amesema kwa kuthibitisha hilo amejenga
nyumba mpya kubwa nyumbani kwao ndani ya miezi mitatu.
“Watu
hawajui kwamba walinipa pesa nyingi sana mpaka leo bado nazitumia, nyie
mnaona kama zimeisha hazijaisha, hapa sasa hivi nawazima kidomo domo
wale... waliosema nimefilisika, sasa hivi najenga nyumba nyingine kijijini
kwangu Moshi na ndani ya miezi mitatu nyumba kubwa imekamilika,” alisema
Mr Nice.
Aliongeza,
“Watu ambao umefilisika watafikiria kujenga sasa hivi?, hamuwaoni
wasanii wenye stress za maisha, kwa hiyo hili ni jibu kwa wale
waliyokuwa wanaongea sana,”
0 comments:
Post a Comment