Msanii
Madee amesimamia usemi wake ambao alishawahi kutungia wimbo wa "Hip Hop
Haiuzi", na kusema hiyo ndiyo sababu kubwa ya yeye kuacha kurap na
kuanza kuimba. Madee
ameyasema hayo kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East
Africa Radio, na kusema kuwa kwake yeye ilikuwa haimlipi ndiyo maana
akaamua kuwaachia wengine.
“Hip hop haiuzi bro, kwangu haiuzi ndio maana nimeiacha, hao inaowalipa waache waendelee kufanya tu”, alisema Madee. Akiongelea harakati zake za muziki, amesema wimbo ambao ulimtoa wa "Kazi Yake Mola" wakati anaurekodi, Ferouz ndiye...
alitakiwa kufanya chorus, lakini alikataa alipogundua kuwa yeye si maarufu (Underground).
“Niliambiwa nitunge wimbo wa majonzi, unaohusu familia ya babu Tale, nikaandika Kazi Yake Mola, wakanipeleka kwa Majani, Majani akamwambia Feruzi afanye chorus, Feruzi akauliza unaimba na nani, aliposikia ni Madee akajikata, sasa siku hiyo nikaenda Majani akaniambia machizi wameimba hii hapa, alafu ikawa poa na nilikuwa hata siwajui, nikawa natamani niwajue (Man Dojo na Domokaya )”, alisema Madee.
Akiongelea kubaki kwake Tip Top mpaka leo ikiwa wengine wamejitoa, Madee alisema nidhamu na uvumilivu ndivyo vilivyomuweka hapo mpaka leo.
“Mi sikuanza kutoka Tip Top, alianza Mb Dog alivyotoa Latifa ndo akatoka, akaja Keysha, akaja Kasim, mi nimekuja dakika za mwisho, ile inatokana na subira, nidhamu ndio inanifanya niko hapa mpaka leo”, alisema Madee.

0 comments:
Post a Comment