skip to main |
skip to sidebar
RICH MAVOKO: SIKUMBUKI HATA KUKUTANA NA GIGGY MONEY WALA KUTOKA NAYE KIMAPENZI
Msanii
Rich Mavoko amekanusha taarifa za kuwahi kuwa na mahusiano na video
queen Gigy Money, ambaye alisema alishawahi kuwa naye akiwa kidato cha
pili.
Akiongea
na East Africa Radio Mavoko amesema taarifa hizo si za kweli, na
hakumbuki hata kuwahi kukutana naye mrembo huyo, achilia mbali kuwa na
mahusiano naye. “Mi
sijawahi kutoka naye, hata siku moja sijawahi, sina... urafiki naye na
wala sijawahi kuongea naye, sijui kama alishawahi kukutana na mimi,
sijaweka kichwani kama nishawahi kukutana nae sikumbuki.
Mavoko
ameendelea kusema "Sijawahi kuwa na skendo za kipumbavu, mi ni mtu
ambaye sijawahi kuwa na upumbavu kama huo, kwanza mi mwenyewe nashangaa
unajua kila kitu, sijawahi kutoka naye sijui mwenyewe anafikiria nini,
siwezi kujua, siwezi kutambua, sijawahi kuelewa nini kilichompelekea
hivyo”, alisema Richi Mavoko.
Hivi
Karibuni video queen huyo alisema alishawahi kuwa na mahusiano na
msanii huyo wakati yupo kidato cha pili, kitu ambacho ni kinyume na
sheria za nchi na hakifai kwa mtu ambaye ni kioo cha jamii.
0 comments:
Post a Comment