skip to main |
skip to sidebar
NAY: MUZIKI WA SASA SIYO UWEZO ILA NI UJANJA UJANJA
Msanii wa muziki wa Hip Hop, Nay wa Mitego amesema muziki wa sasa hivi
ukileta ufundi na kujifanya unaweza sana kuchana na kuandika hautafika
popote.
Nay wa Mitego amedai ili kwenda kibiashara msanii unatakiwa kubadilika ili
kwenda sambamba na mahitaji ya soko.
“Muziki wa kipindi cha nyuma ulikuwa wa serious sana, ulikuwa unahitaji
uumize sana kichwa ili ufanye kitu kizuri japo...
ulikuwa hauna hela, lakini
muziki wa sasa hivi ni muziki wa ujanja ujanja mwingi, ukiwa na akili
nyingi, ukiwa mjanja basi unamake mkwanja.
Kwa
hiyo naweza nikasema muziki wa sasa hivi una hela sana kuliko wa zamani
lakini ili uzipate unatakiwa kuwa mjanja, unaweza ukawa unachana sana,
unaandika sana lakini ukatoka bila,” alisema Nay.
Aliongeza, “Muziki wa sasa hivi ukidumu
kwa muda mrefu ni miezi mitatu, lakini nyimbo nyingi za zamani
zitaendelea kuwepo kwa sababu wasanii wake walikuwa hawana ujanja
ujanja, wanaandika kweli na wanazingatia kila kitu katika uandishi,”
alisema Nay.
0 comments:
Post a Comment