Mkali wa ‘Ligi ndogo’ Bill Nas amesema wasanii wengi wa Hip Hop wanashindwa kufanya vizuri kutokana na mfumo wa muziki nchini kuwapa nafasi zaidi wasanii wa muziki wa kuimba.
Akizungumza
na Bongo5 Jumatano hii, Bill Nas alisema hali hiyo imewafanya wasanii wa Hip
Hop wazidiwe nguvu na wale wa kuimba. “Tatizo
kubwa ambalo mimi naliona ni mfumo tu wa muziki wetu. Kwa sababu...
ukimzungumzia
mtu kama County Boy, Young Killer, Stamina mimi naamini wote wana uwezo mkubwa,
lakini muziki ulivyo ndiyo unafanya waonekana wakawaida,” alisema Bill Nas
Aliongeza,
“Kiukweli hata mimi naona muziki wa Hip Hop haufanyi vizuri kabisa. Tumeona
wasanii wa Hip Hop sasa hivi wanafanya nyimbo kali, video kali lakini
tunazidiwa kwenye nguvu. Mimi naamini nguvu imebadilika, zamani ulikuwa
ukimzungumzia Professor Jay hakuna msanii wowote wa kuimba unaweza
kumlinganisha nae kwa ukubwa. Kwahiyo kwetu sisi nikinyume, waimbaji wamekuwa
na nguvu kubwa kuliko watu wa Hip Hop, na hii imetokana na wasikilizaji
wanapewa sana muziki wa kuimba kuliko Hip Hop.”
0 comments:
Post a Comment