Ilifahamika kuwa mastaa wawili wa Bongo Movie Wema Sepetu na Aunty Ezekiel hawana mahusiano mazuri, na hiyo ni baada tu ya mahusiano ya kimapenzi ya Diamond Platnumz na mwanadada Wema Sepetu kusitishwa na kutokea hali ya sintofahamu kwa mwanadada Aunty Ezekiel atajikita zaidi na upande gani ikiwa yeye ni baby mama wa dancer wa Diamond Mose Iyobo.
Unachotakiwa kukifanya ni kufuta kabisa fikra hizo katika kichwa chako, kwasababu madame Wema Sepetu ameamua kukata utepe kuhusiana na...
suala hilo.
Picha lilianza kwa mwanadada Wema Sepetu kutupia picha ya Aunty Ezekiel akiwa na mwanae Cookie katika ukurasa wake wa Instagram na kuandika kuwa hiyo ndio picha yake ya siku.
Maneno hayo yalitoa taswira kuwa hakuna tena tatizo ndani ya moyo wa mwanadada Wema juu ya Aunty. Kila la kheri kwa wawili hawa.
0 comments:
Post a Comment