Mkazi wa Kijiji cha Lindusi Peramiho mkoani Ruvuma aliyejichongea
jeneza, Scholastica Mhagama amefariki dunia kwa ugonjwa wa pumu, Mapema mwaka huu wakati alipohojiwa, bibi huyo alitaja
sababu za kujichongea jeneza kabla ya kifo kuwa, ni kuhofia kuzikwa
kama mnyama baada ya kuwa na ugomvi wa mara kwa mara na kaka zake.
Kaka yake mkubwa aliyekuwa akimhudumia kabla ya kufariki dunia, Felix
Mhagama (82) alisema dada yake alikufa Jumanne ya wiki iliyopita kwa
ugonjwa huo, Mhagama alisema licha ya kipindi cha uhai wa dada yao, kugombana mara kwa mara walikuwa...
wakipatana na kumaliza tofauti zao.
“Ingawa mdogo wangu alikuwa na upungufu niliendelea kuzungumza naye
na kumhudumia, kwani hakuwa na uwezo wa fedha na alinitegemea kwa kila
kitu,” alisema. Alisema alikuwa akiumia kuona dada yake akiishi na
jeneza hilo na kwamba, kuna wakati alimuuliza sababu za kufanya hivyo,
alimjibu kuwa ni kutokana na kutokuelewana kwao.
Alibainisha kuwa kabla ya kifo chake, kuna watu walikwenda nyumbani
kwake na kuvunja jeneza hilo na kuahidi kumtengenezea jingine.
Kuhusu chanzo cha ugomvi wa Scholastica na kaka zake, jirani yao,
Cassian Kazimoto alisema alikata tamaa ya kuishi kutokana na maradhi
hayo ya pumu yaliyokuwa yakimsumbua na ulemavu baada ya kukatwa mguu.
Saturday, October 29, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment