Pages

Subscribe:

Tuesday, November 1, 2016

MR BLUE: MKE WANGU ANAWIVU MPAKA ANAKUWA MWEKUNDU

mrbluebyser1988-20161029-0001
Rapa ambaye amesimama kwenye game la muziki wa Bongo flava kwa miaka mingi sasa, Mr Blue amethibitisha kuwa mke wake anawivu sana hadi anakuwa mwekundu.
Akizungumza hili kwenye FNL, Mr Blue alisema hayo baada ya kuulizwa kuhusu kuwa karibu sana na video queen aliyemtumia kwenye video ya wimbo wa Baki na Mimi kwa kuwa naye karibu sana.

“Mke wangu anawivu vibaya mno hadi anakuwa mwekundu kabisa, Ukiona ivyo inabidi niage kabisa, Ile video ya Baki na mimi, video queen aliye husika ni ndugu na kaka yangu hivyo mke wangu alikuwa...
anaelewa japokuwa alituma watu kuja kuchungulia nini kinaendelea.” Alijibu Mr Blue.

Mbali na hilo, Mr Blue alisema kuwa kwasasa yeye hafanyi tena muziki kama uhuni kwakuwa anazeeka na watoto wake kwa sasa wanakuwa, Hivyo anafanya muziki kama kazi.

0 comments:

Post a Comment