Pages

Subscribe:

Wednesday, December 7, 2016

BEN POL: MUZIKI YA DARASSA ILIREKODIWA KAMA MASIHARA HIVI


“Maisha na Muziki” ni ngoma ambayo imedropishwa kwa kipindi kifupi na kuweza kupenya hadi kufikia hisia ya kila mtu yaani “muziki” imekuwa ni ngoma flani hivi amaizing ambayo sasa hivi kila ukipita sehemu kila mtu utasikia maisha na Muziki. 

Sasa kama ulikuwa ni mfuatiliaji wa karibu katika kurasa ya Twitter ya Ben Pol, umeweza kujionea jinsi anavyo weza kueleza hisia zake tofauti tofauti kuhusu Joint ya “Muziki”.
Hapa juzi kati Ben Pol alifunguka na kusema kwamba pindi siku mtu unaamua kurekodi ngoma ile serious linakosa...
mashiko, ila cha kushangaza zaidi ni kwamba ngoma ya Muziki ambayo Ben Pol ameisimamia vizuri amefunguka na kusema kwamba wakati wanarekodi wimbo huo ilikuwa ni kama masihara hivi.

Leo kupitia kurasa yake ya Twitter Ben Pol katoa kali nyingine kuhusiana na ngoma hiyo, Ben ametweet: Ukitaka kutoa wimbo kipindi hiki kwanza “chek kushoto, check kulia” maana Darassa kaweka msuli, featuring mimi by d way.
Kwa mtazamo huo, ina maana Darassa kaamua kuwanyoosha this time, hahahaha natania. kikubwa ni mziki mzuri utabaki kuwa mzuri.

0 comments:

Post a Comment