Staa wa muziki wa Bongo Fleva, Juma Mussa a.k.a Jux imeonekana kuwa alikuwa akitoa simulizi za kimahaba katika nyimbo zake hata kusemekana kuwa upo uwezekano kuwa alitabiri kilichotokea katika mahusiano yake ya kimapenzi na Muimbaji Staa wa muziki wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee.
Kwa mujibu wa mtiririko wa kazi zake ndani ya kipindi cha miaka mitatu mpaka minne, Jux ameonekana kusimulia mtiririko wa matukio ya kimapenzi ikishabiliana na hali yake kimahusiano na Vanessa Mdee. Mwishoni mwa mwaka 2013 Jux aliachia...
wimbo uliokwenda kwa jina ‘Uzuri wako’ uliobeba wazo la kuusifia uzuri wa mrembo wake mwaka ambao haikuwa imethibitka kuwa tayari walishaingia katika mahusiano mazito.
Mbali na tetesi kutembea kwa kipindi huku wao wakikana kuwa katika mahusiano, Jux akiwa katika hali ya kuipromote kazi ya ‘Nikuite Nani’ mitandaoni zilianza kupita pita picha zao wakiwa pamoja katika mapozi kwa kupokezana ambayo kwa asilimia kubwa mtu ungekubali kuwa wawili hao ni zaidi ya urafiki wa kwaida kati ya mwanamke na mwanaume.
Jux katika picha ya pamoja na wahitimu wezake nchini China
Katika simulizi ya wimbo huo wa Jux utagundua kuna hali ya kutolewana, kuvunjika kwa penzi kisha kusameheana na kurudiana kwa wapenzi(Jux na Vanessa) kitu ambacho mpaka sasa hakijatokea kwa wawili hao na zaidi mashabiki wanaishia kubembeleza na kutamani penzi la wawili hao kurudi ili iwe kama zamani.
Hata hivyo mabli na uchunguzi huu wa kupitia kile kinachoweza na ushabiliano wa amisha mafupi ya kimahusiano kwa Jux na Vanessa Mdee, bado wawili hao hawajaonesha dalili za kurudiana zaidi ya kuonekana katika majukwaa wakitumbuisha baadhi ya nyimbo ambazo ziliwakutanisha kwa namna moja au nyingine ukiwemo wimbo wa ‘Juu’ uliowakutanisha kwa mistari ya kujibizana kwa maneno ya kupendana na kufurahia ukaribu wao.
0 comments:
Post a Comment