Klabu ya Yanga imefanikiwa kunasa saini ya beki wa kati, Fiston
‘Festo’ Kayembe Kanku kutoka klabu ya Balende FC ya DR Congo kwa
mkataba wa miaka miwili.
kocha mkuu wa timu hiyo Mzambia, George Lwandamina.
“Fiston ‘Festo’ Kayembe Kanku amesaini mkataba wa miaka miwili kujiunga na Mabingwa mara 27 Yanga akitokea Balende FC ya DR CONGO. Festo anayeimudu vyema nafasi ya mlinzi wa kati amefanikiwa kusaini kandarasi hiyo baada ya majuma kadhaa ya majaribio chini ya kocha George Lwandamina.”
Usajili wa Kayembe unakuja muda mfupi baada ya Yanga jana kuruhusu
goli la tano kwenye ligi kuu msimu huu ambalo lilipelekea timu hiyo
kulazimishwa sare ya 1-1 na Tanzania Prisons kunako dimba la uwanja wa
Azam Complex, Chamazi.



Follow on Instagram
0 comments:
Post a Comment