Kila
nchi uwa na stori zake ambazo ushika headlines na kuchukua mijadala
katika maeneo mbalimbali ya nchi hasa kwenye vijiwe vya stori sasa
nikusogezee hii ambayo imeshika headlines Jana na Leo January 12, 2018 nchini
Sri Lanka ambapo serikali imewaruhusu wanawake waliotimiza umri wa miaka
18 kununua pombe na kunywa kwa mara ya kwanza katika kipindi cha zaidi
ya miaka 60.
maana kwamba wanawake wataruhusiwa kufanya kazi katika maduka na sehemu zinazouzwa pombe bila kuhitaji kuwa na kibali.
Wanawake wengi wamefurahia mabadiliko hayo na kutoa shukrani kwa serikali ya nchi hiyo. Kwenye sheria mpya iliyotangazwa na waziri wa fedha Mangala Samaraweera wanawake hawatahitaji ruhusa kutoka kwa kamishna wa forodha kufanya kazi au kunywa pombe katika maeneo yaliyoidhinishwa, ikiwa ni pamoja na baa.
0 comments:
Post a Comment