Rapper huyo ameiambia Planet Bongo ya EA Radio kuwa kitu hicho si kizuri kwani licha ya kuua muziki inaweka uzibe kwa wasanii wachanga. “Hiyo kitu ni zuluma, ni utapeli yaani vitu ambavyo...
havitakiwa kuwepo na ni kweli hiyo system ipo Tanzania muda huu, nasikia ukitaka interview utoe hela, ili wimbo wako uchezwe utoe hela,” amesema JCB.
JCB ameongeza kuwa kutokana na tabia hiyo kuanza kushamiri ndio sababu miaka ya hivi karibuni hakuna msanii underground aliyetoka na kufanya vizuri bali wanaosikika ni wale wale ambao tayari wanajuana na baadhi ya watu katika vyombo vya habari.
0 comments:
Post a Comment