“Bado hatajupanga hilo lakini tunarekodi nyimbo, mara nyingi sisi wasanii tunakuwa tupo pamoja, tunatembea pamoja, pengine kama tutakaa sawa na menejimenti ya Vanessa na team yangu kwa sababu nje ya...
mahusiano yetu ni kazi pia,” amesema Jux.
“Kwa hiyo tunaweza tukasema tunaweza tukatoa albamu ya pamoja lakini siyo vitu ambavyo vipo tayari, ni mipango ambayo inaweza kuja baadaye,” amesisitiza.
Jux na Vanessa wameshatoa ngoma moja ya pamoja inayokwenda kwa jina la Juu, pia walishirikishwa na Nikki wa Pili katika wimbo ‘Safari’ ambao uliwakutanisha wasanii wengine kama Joh Makini, G Nako na Navy Kenzo.



Follow on Instagram
0 comments:
Post a Comment