Pages

Subscribe:

Monday, January 1, 2018

STORY; MPAKA KIELEWEKE (Sehemu Ya Nne) 04

Image result for salem village
“Shikamoo mzee, sijui wewe ndo mzee Miale?” nilisalimia akaitikia nikamuuliza na swali ambalo alilijibu kwa kukubali kuwa ndio yeye, nami nikajitambulisha na akanitambua haraka kwa maana alikua tayari ameshaelezwa juu yangu, alinichukua tukaingia ndani kisha akaanza kunieleza juu ya ambacho kimemtokea mke wangu, akianzia kunipa historia ya miaka mingi sana iliyopita.

“Zamani eneo hili lilikuwa ni himaya ya wachawi wenye nguvu kubwa sana, wachawi kutoka maeneo mbalimbali walikuja katika eneo hili na kujifunza taaluma hiyo kisha wakatoka wakiwa na...

uwezo mkubwa sana.

Wachawi hao walikwenda kwenye maeneo yao na kuwa wasumbufu katika jamii, na kama nilivyokueleza walikuwa na nguvu sana hivyo mbinu za kupambana nao hazikuwa zikifanikiwa. 


Ulifikia wakati watawala wa maeneo mbalimbali walikutana na kujaribu kushauriana nini kifanyike juu ya wachawi ambao walikuwa kero kubwa kwa wananchi wa himaya zao, tawala zile zikakubaliana kuwa eneo hili ambalo ndilo lilikuwa makao makuu ya shughuli hizo haramu liteketezwe lote, mipango ikapangwa wakishirikiana na waganga wa kienyeji ambao walikuwa na mbinu za ziada na ikabainika siku ambayo wachawi wote hukutana katika eneo lile, wakaamua kuitumia siku hiyo kwenda kuwateketeza wote, lakini kwa bahati mbaya habari zikavuja na kuwafikia wachawi wale ambao waliutumia uchawi wao kujikinga.

Wakajenga himaya yao ndani ya eneo hili kisha wakafanya zindiko kubwa kuhakikisha himaya yao hiyo haitokuwa ikionekana na mtu yeyote, hivyo watu wale waliokwenda kwa ajili ya kuwateketeza walikuta mji huu hauna mtu hata mmoja, ikabidi wataalamu ambao walikua nao wapige ramli na kugundua nini kilikua kimetokea, wakagundua zindiko hilo la wachawi hivyo nao wakafanya ufundi wao kuzuia himaya hiyo ya siri ibaki hukohuko na isiingiliane na himaya hii, kisha wakafanya utaalamu mwingine ili watu wa himaya hiyo ya siri wasizaliane wakiamini watakuwa wakifa bila kuzaliana hatimaye himaya hiyo itatoweka.

maisha yakaenda hivyo kwa muda kidogo lakini baadae watu wa himaya ile ya kichawi wakapata namna ya kuwa wanapenya na kuja himaya hii mara chache.

Baadae wakaamua kuwa ikitokea mtu amekufa himayani mwao basi hutoka nje ya himaya yao na kumchukua mtu mwingine ili aende kuziba nafasi ile, lakini ilikuwa ngumu sana kwa mtu ambaye ametokea huku nje kuishi kama ambavyo wao walitaka hivyo wakaja kugundua njia nyepesi na kumfanya mtu awe wa kule (mtu wao) na kisha aishi kama wao ni mtu huyo kuzaliwa katika ardhi yao. 


kwa kua hawakuweza kuzaliana kutokana na laana ile ya wazee wa zamani wakaamua kua wawe wanakuja huku na kukamata wanawake wajawazito kisha wanawapeleka katika ardhi yao ili mtoto akazaliwe katika ardhi yao na kisha hua wa kwao kabisa.. ”alitulia kidogo akaniuliza, “ni kweli mkeo alikuwa mjamzito??”, nami nikamjibu kua ni kweli, mke wangu alikuwa na ujauzito wa miezi miwili.

Sasa nilikuwa nimejua nini kilikuwa kimempata mke wangu.
“nawezaje kumpata mke wangu mzee?” nilimuuliza mzee Miale huku moyoni nikiwa nasali kuwe na njia ya kufanikisha hilo.

Usikose sehemu ya tano

0 comments:

Post a Comment