Pages

Subscribe:

Saturday, January 13, 2018

STORY: NALIA NA NAFSI YANGU (Sehemu Ya 16) - 16

Related image
Sehemu ya:16
Mtunzi: Agatha Francis

Mama Prisca alilia sana, alilia mpaka kamasi zilitoka, kama ujuavyo mpenzi msomaji jaribu kufikiria ndiyo uzao wako wa kwanza alafu unazaa mtoto anapatwa na hali hiyo, inaumiza sana. Basi Mark yeye ndiye aliyekua na kazi yakuwabembeleza kwani hata Baraka aliishiwa nguvu, kila alipomtazama mwanae alipatwa na uchungu, alilia sana, daktari aliwahurumia sana kwani ni kweli iliumiza sana hali ya majibu ya mtoto Prisca. 


Basi daktari aliandika tena barua na kuwaomba warudi mapema kijijini, waende hospitali na wairudishe ile barua ili mtoto aanze tiba mapema. Mama Prisca na ndugu zake walianza...
kurudi nyumbani wakachukue mizigo yao ili siku ileile waondoke, mama Prisca alilia njia nzima kiasi kwamba watu walimshangaa, kuna waliohisi kafiwa na mtoto ambaye alibebwa na Mark akiwa kafunikizwa nguo. Mark alimuhurumia sana dada yake na shemeji yake lakini hakua na lakusema zaidi aliwatia moyo ndugu zake. 

Walifika nyumbani walikuta Suzy anaangalia runinga sebuleni, wala hakushtushwa na kilio cha wifi yake, Suzy akasema"karibuni, mbona vilio, za mtokako", aliongea huku akiendelea kuangalia runinga, Baraka alitikisa kichwa tu kisha Mark alijibu "nzuri", basi Suzy aliinuka na kuelekea chumbani. 

Baraka akasema"shemeji yangu najua utalaumu sana dada yako kwani hapa hauna mke, natamani niseme kaishi na mama Careen lakini ndiyo basi tena", Mark akajibu "wala usijali shemeji yote haya aliyataka dada mimi nilimpenda mama Careen lakini uliona alichofanya dada yangu, shemeji huu muda sio wakuzungumzia habari hizi ni kitendo cha ninyi kujiandaa na safari mrudi kijijini", Mark alisema, mama Prisca hakua na lakusema alionekana kuchanganyikiwa kabisa. Mark aliwaandaa ndugu zake na kuwapa kiasi cha pesa pia aliwasisitiza kumueleza kila linaloendelea kwani mtoto ili akue vizuri anahitaji kula vizuri. 

Baraka alishukuru sana na walimuambia Mark utatuagia mkeo sisi tunaondoka ila ikiwezekana mrudie mama Careen kwani huyu uliyenaye sio mwanamke hata kidogo ndugu yangu, Mark akajibu"usijali kwani mama Careen tunawasiliana vizuri tu na nikienda nitamwambia kama mlikuaja", Baraka akasema "tuombee msamaha pia", 
usikose 17

0 comments:

Post a Comment