Ilikuwa majira ya saa 2:00 usiku kwenye uwanja wa Mfalme Abdullah jijini Jedda, wanawake walikuwa tayari uwanjani wakitazama mechi ya ligi kuu kati ya Al-Ahli dhidi ya Al-Batin ambapo Al Ahli ilishinda mabao 5-0 na kuendelea...
kusalia katika nafasi ya 2 kwenye msimamo wa ligi hiyo yenye timu 14 huku Al-Batin ikibaki katika nafasi ya tisa.
Ruhusa ya wanawake kuingia uwanjani ilitolewa mwezi Oktoba mwaka jana na Mtawala wa sasa wa nchi hiyo (Crown Prince Mohammad Bin Salman Al Saud) ikiwa ni sehemu ya mabadiliko makubwa yanayofanyika nchini humo yanayolenga kuleta haki na usawa kati ya mwanamke na mwanaume katika baadhi ya maeneo.
Hata hivyo wanawake wametengewa jukwaa lao "Family sections" ambapo
wataruhusiwa kukaa na familia zao bila kuchanganyikana na wanaume ambao
si wa familia zao. Baada ya mechi ya jana usiku pia kesho kutakuwa na
mechi kwenye uwanja wa Mfalme Fahd jijini Riyadh ambapo pia wametengewa
jukwaa maalum.Alhamisi ijayo pia wanawake watapata nafasi ya kuhudhuria mechi kwenye uwanja wa Prince Mohammed bin Fahd mjini Dammam wakiketi na familia zao kama ilivyokuwa jana. Mwaka jana pia serikali ilitoa ruhusa ya wanawake kuanza kuendesha gari katika shughuli zao mbalimbali za kila siku.



Follow on Instagram
0 comments:
Post a Comment