skip to main |
skip to sidebar
LULU AWASHAURI WATU WAACHANE NAMATUMIZI MABAYA YA MITANDAO YA KIJAMII
Muigizaji wa filamu, Elizabeth ‘Lulu’ Michael anaamini hawezi kufikia
malengo yake kwa mawazo yake pekee bali anahitaji msaada kutoka kwa
vijana wenzake ambao nao wana nia na malengo kama yake katika kufikia
ndoto zao. Ndio maana anahisi Instagram inaweza kuwa ni sehemu nzuri ya
vijana kupenda michongo na sio matusi. Lulu alisema...
“Nikiwa Kama Kijana Mpenda Maendeleo, mwenye ndoto na malengo ya
kufika mbali najua mawazo yangu peke yangu yanaweza yasitoshe mimi
kufika ninapopataka,” ameandika kwenye Instagram.
“Najua wapo vijana wengi wenye nia kama yangu..!Nadhani umefika
wakati wa kutumia mitandao ya kijamii Kwa kujengana na kusaidiana hasa
ki mawazo Ili wote tuweze Kuwa sehemu fulani siku moja.”
Lulu ameonesha wazi kuwa hapendezwi na tabia ya baadhi ya watu ambao
wamekuwa wakitumia mitandao ya kijamii vibaya hasa kwa kudhalilishana.
0 comments:
Post a Comment