skip to main |
skip to sidebar
NAY AELEZA SABABU YA KUINUNUA SANAMU YA SHETANI KWA SH. MILLION 5
Nay wa Mitego ni mtu wa maamuzi na mapenzi tofauti na wengine. Ndio maana
ukiingia ndani kwake utakutana na sanamu isiyo ya kawaida – ni sanamu ya
shetani!
Rapper huyo ameiambia Bongo5 kuwa sanamu hiyo ni moja ya vitu anavyovipenda
zaidi ndani mwake.
“Mimi naipenda na niliinunua hela nyingi tu, ni dola elfu tatu,” amesema
Nay.
“Nilitokea tu kuipenda, ni moja kati ya... vitu muhimu ninavyovipenda ndani ya
nyumba yangu. Kuna sehemu niliinunua sio Tanzania. “Mimi nilitokea
kukipenda yaani naipenda sana tena sana na hata ukiingia ndani kwangu
utaanza kuiona hiyo,” amesisitiza rapper huyo.
0 comments:
Post a Comment