Taasisi ya afya ya kimarekani (NIH) imetangaza kufanyika kwa
majaribio ya chanjo mpya ya ukimwi nchini Afrika Kusini chini ya njia
yake mpya inayoitwa HVTN 702, kupitia chanjo inayofahamika kwa jina la
PILOT ACQUIRED IMMUNE DEFICIENCY SYNDROME VACCINE, chanjo inayoonekana
kuwa na... mafanikio zaidi kuliko chanjo nyingine zote zilizowahi
kugundulika.
Katika
taarifa iliyotolewa na taasisi hiyo,wamedai kuwa”Kwa mara ya kwanza
katika miaka saba, jamii ya wanasayansi imekua katika majaribio
makubwa ya chanjo ya kukabiliana na Virusi vya Ukimwi (VVU),na
kufanikiwa kupatikana kwa chanjo hii,ikiwa ni matunda ya miaka mingi ya
utafiti na majaribio,” alisema Dk Anthony Fauci, mkurugenzi wa Taasisi
ya Taifa ya Allergy na Magonjwa ya kuambukiza (NIAID), ambayo ni sehemu
ya Taasisi ya N.I.H.
Majaribio ya chanjo hiyo yataanza kufanyika mwezi November katika
majiji 15 nchini Afrika Kusini,hii ikiwa ni baada ya chanjo hiyo kutibu
asilimia 34 ya watu walipewa chanjo hiyo nchini Thailand mwaka
2009,ambapo katika majaribio ya chanjo hii nchini Africa kusini,taasisi
hiyo imepanga kuwapa chanjo hiyo zaidi ya watu 5,400 wanaume kwa
wanawake wenye umri kati ya miaka 18 hadi 35 hasa wale walio kwenye
mazingira hatarishi ya kupata virusi vya ukimwi,huku majibu rasmi ya
matokea ya chanjo hiyo yakitarajiwa kutoka mwaka 2020.
0 comments:
Post a Comment