Hatahivyo, alipigwa faini ya dola 3,700 baada ya jaji kuamuru hakuvunja sheria kwa kusambaza data ya uke wake ambayo inaweza kutumika kutengeza umbo la uke wake. Sheria kali za Japan zinapinga kuonyeshwa... hadharini kwa sehemu za siri.
Igarashi mwenye umri wa miaka 42, kwa jina Rokudenashiko au ”good for nothing girl” alikamatwa mwaka 2014 baada ya boti yake kuonyeshwa katika duka moja la vifaa vya ngono mjini Tokyo.
Alishtakiwa chini ya sheria ya mambo machafu kwa kuonyesha boti hiyo na kusambaza data yake kwa wale waliochangisha fedha ili itengezwe. Siku ya Jumatatu jaji mmoja aliamua kwamba rangi zake zinazong’aa na mapambo yake hayaonyeshi ukweli wa umbo la uke.
“Lakini data yake licha ya kutokuwa na umbo la uke itatumika kutengeza uke wa Bi Igarashi kwa kutumia 3D na hivyobasi ni uchafu,” alisema jaji.
Bi Igarashi alipigwa faini nusu ya Yen 800,000 zilizohitajika na afisi ya mashtaka.
0 comments:
Post a Comment