skip to main |
skip to sidebar
MARUFUKU KUVAA NGUO FUPI SHERIA ZA VIBOKO NA FAINI ZATAJWA
Moja ya matukio ambayo yanamake headlines katika Wilayani Siha
Kilimanjaro ni pamoja na adhabu zinazotolewa kwa wale wanaovunja sheria,
kingine ni kwamba kijiji cha Sanya Hoye kimepitisha adhabu ya faini ya
Shilingi 50,000 pamoja na viboko 15 kwa atakayekutwa baa na mtoto mdogo
au kuvaa nguo fupi.
Mwenyekiti wa kijiji cha Sanya Hoye, Moses Mnuo ametoa ufafanuzi wa
maazimio waliyokubaliana katika kikao cha kijiji cha Sanya Hoye. ‘Tumepitisha sheria kwa mtu yeyote anayevaa nguo fupi kwa watoto wa kike
ni... marufuku tangu siku ile ya kikao kile, wanawake hao wanapotembea
hapa usiku wana ajenda walizonazo wanafanya machafu yao kwa hiyo
tutawapiga faini na hizo hela watapewa risiti’
0 comments:
Post a Comment