skip to main |
skip to sidebar
NAJ: SIJALI BARAKAH DA PRINCE AMETOKA NA WANGAPI HAPA NAHISI NIMEFIKA
Mwanamuziki Najma Dattan ‘Naj’ ameibuka na kusema kuwa kwa msanii
mwenzake Baraka Da Prince amefika wala hajali ametoka na wanawake
wangapi kwa sababu hata yeye ana ‘pasti’ yake. Najma alisema kuwa amekuwa akiwashangaa wasichana
waliopita kwa Baraka ndiyo wanamuongelea... kila siku wakidai anakula
makombo lakini Baraka mwenyewe haongelei kabisa uhusiano wa watu wake wa
zamani.
“Sijali ametoka na wangapi, hayo ni maisha ambayo kila mtu anapitia.
Niseme tu kwamba sijawahi kumtambulisha mwanaume kwetu, hapa kwa Baraka
nahisi nimefika kwa sababu ndiye mwenye penzi la kweli, kitakachofuata
muda si mrefu ni ndoa tu kwani wazazi wetu wanaujua uhusiano wetu,”
alisema Najma.
0 comments:
Post a Comment