Pages

Subscribe:

Tuesday, October 4, 2016

MADEE: MANZESE INGEKUWA BORA KAMA NINGEKUWA DIWANI


Msanii Madee leo amefunguka mipango yake iwapo angepata fursa ya kuwa kiongozi kwenye jamii anayotokea ya Manzese, na kusema kuwa ndoto yake kubwa ilikuwa kuwaletea mandeleo watu wa Manzese.

Akizungumza kutoka Manzese Dar es Salaam, Madee amesema kwa sasa Manzese imekua kutokana na kuongezeka kwa watu, hivyo ndoto yake kubwa ilikuwa kuwaletea huduma bora wakazi wa Manzese, pamoja na...
kusaidia kutatua tatizo la ajira kwa vijana.

"Unajua Manzese sasa hivi ina watu wengi, kila kukicha watu wanahamia, sehemu yenye watu wengi ndiyo sehemu ya kuweka huduma bora za jamii, ningekuwa na nafasi hata ya udiwani, ningejitahidi kuhakikisha huduma bora za jamii zinapatikana, vijana wote wa Manzese wangetafutiwa ajira waache masuala ya kukaa vijiweni", alisema Madee.

Madee aliendelea kusema kuwa anafurahishwa na serikali ya sasa kuwaacha vijana wa maeneo hayo kufanya biashara ndogo ndogo maarufu kama wamachinga, kwani imesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza tatizo la ajira na vijana kutoka maskani.
"Mwanzo walikuwa wanabughudhiwa sana lakini sasa hivi naona serikali imeaachia kwa sababu wameona ni vijana ambao hawataki kujihusisha na ukabaji, so naipa big up kwa hilo", alisema Madee.

0 comments:

Post a Comment