Pages

Subscribe:

Friday, October 7, 2016

MR NICE AVAMIWA NA MAJAMBAZI AIBIWA MALI ZAKE NA KUPORWA MILLIONI 30

img-20161007-wa0008
Mwanamuziki, Lucas Mkenda ‘Mr Nice’ hivi karibuni amedai alivamiwa na majambazi akiwa nchini Kenya na kuibiwa simu 2, laptop, pamoja na pesa taslimu kiasi cha tsh milioni 30.Muimbaji huyo kwa sasa yupo nchini Kenya kwa zaidi ya miezi 6 akifanya shughuli za muziki pamoja na show.

Akiongea na Bongo5 Ijumaa hii akiwa nchini Kenya, Mr Nice amesema alivamiwa na majambazi hao akiwa katika apartment ambayo amekodiwa na kampuni ambayo...
inamtafutia show.

“Nilivamiwa na majambazi wakaniibia kila kitu na pesa taslimu kama 1.7ksh ambayo ni zaidi ya million 30 za kibongo, gari yangu ikavunjwa vunjwa vioo, laptop, simu mbili, nguo na viatu vyote wakabeba, hadi passport ilikuwa kwenye begi walilobebea nguo nayo ikaenda,” alisema Mr Nice. 

“Ilikuwa hatari sana maana walikuwa wengi kama 7 na wawili walikuwa na bunduki kubwa kabisa, hata nilishtuka sana nikijua ni alshabaab lakini baada ya kuchukua vitu na kutokomea nikajua ni majambazi tu,”

Aliongeza, “Nashukuru hawakunidhuru mahali popote ila pia kwa staili waliyoniingilia nayo inaonekana ni kama walikuwa wameelekezwa kuwa nilikuwa na pesa maana ni jioni hiyo tu nilikuwa nimetoka kuchukua hela ya shows na ilikuwa kama saa 11 jioni, So sikuwa na mahali pakuzipeleka zaidi ya kuzihifadhi hadi ifike kesho yake, kwa hiyo sisi tunaingia kwenye geti la tunapoishi tunashangaa na wao wakiingia na mapikipiki, wakafanya yao wakaondoka,”

Pia amesema jeshi la Kenya linaendelea kuchunguza kuhusiana na tukio hilo ambalo lilitaka kuhatarisha maisha yake.
“Nashukuru serikali ya Kenya, police pia wanaendelea kuchunguza tukio. Pia ninaomba kama kuna raia yoyote ataokota documents zangu za kusafiria anisaidie kwa kuziwasilisha sehemu ambayo nitaweza kuzipata ama kituo chochote cha police, so far niko poa na ninaendelea na tour yangu kama kawaida na kila kitu kiko shwari,”

Pia muimbaji huyo amesema baada ya tukio hilo kwa sasa anaendelea na show zake katika sehemu mbalmbali za Kenya huku akidai mambo ameanza kumnyookea zaidi.

0 comments:

Post a Comment